Isaya 25 - Swahili Congo Revised Bible 2002

Wimbo wa sifa kwa Mungu

1Wewe, ee Yawe, ndiwe Mungu wangu;

nitakutukuza na kulisifu jina lako,

kwa maana umetenda mambo ya ajabu;

unaitimiza kwa uaminifu na kweli

mipango uliyoipanga tangu zamani.

2Umeufanya muji kuwa lundo la mawe,

muji wenye pango kuwa uharibifu.

Nyumba za watu wageni zimetoweka,

wala hazitajengwa tena upya.

3Kwa hiyo watu wenye nguvu watakutukuza,

miji ya mataifa kali itakuogopa.

4Maana wewe umekuwa kimbilio kwa wazaifu,

pango kwa wakosefu katika taabu zao.

Wewe ni kimbilio wakati wa zoruba,

kivuli wakati wa joto kali.

Kweli pigo la watu wakali ni kali

kama zoruba inayopiga ukuta;

5ni kama joto la jua juu ya inchi kavu.

Lakini wewe unakomesha fujo ya wageni.

Kama wingu linavyofifisha joto la jua,

ndivyo unavyokomesha nyimbo za ushindi za watu wakali.

6Juu ya mulima Sayuni, Yawe wa majeshi atawafanyia watu wote karamu ya nyama zenye kunona na divai nzuri, nyama tamu zenye mafuta, pamoja na divai safi.

7Katika mulima huuhuu, Yawe ataliondoa wingu la huzuni lililowafunika watu wote, kifuniko cha uchungu juu ya mataifa yote.

8Bwana wetu Yawe atakiangamiza kifo milele! Atayafuta machozi katika nyuso za watu wote na kuondoa haya ya watu wake katika dunia yote. Yawe amesema hivyo.

9Siku ile, watu wote watasema: Huyu ndiye Mungu wetu! Tumemungojea atuokoe. Huyu ndiye Yawe tuliyemutazamia. Mukuje tufurahi na kushangilia kwa sababu ametuokoa.

Mungu ataiazibu Moabu

10Yawe ataulinda mulima wa Sayuni, lakini watu wa Moabu watakanyagwakanyagwa ndani ya inchi yao kama nyasi katika shimo la mboleo. Ang. Isa 15.1–16.14; Yer 48.1-47; Eze 25.8-11; Amo 2.1-3; Zef 2.8-11

11Watainyoosha mikono yao kama mutu anayejaribu kuogelea, lakini pamoja na bidii yao, Yawe ataporomosha kiburi chao.

12Atabomoa pango za miji ya Moabu yenye kuta ndefu na kuiangusha chini ndani ya mavumbi.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help