Yobu 23 - Swahili Congo Revised Bible 2002

1Kisha Yobu akajibu:

2Hata leo malalamiko yangu ni ya uchungu.

Ninapata maumivu na kuugua.

3Heri ningejua pahali nitakapomupata Mungu!

Ningeweza kwenda hata karibu naye.

4Ningeleta maneno yangu mbele yake,

na kumutolea utetezi wangu.

5Ningeweza kujua atakachonijibu,

na kuelewa atakachoniambia.

6Angeshindana nami kwa nguvu zake zote?

Hapana! Bila shaka angenisikiliza.

7Pale, mutu wa usawa anaweza kujitetea.

Mungu, mwamuzi wangu angeamua kuwa sina kosa milele.

8Ninakwenda mbele, lakini simupati;

ninarudi nyuma, lakini siwezi kumwona.

9Ninamutafuta upande wa kushoto lakini simwoni;

ninageukia upande wa kuume, lakini siwezi kumwona.

10Lakini yeye anajua njia ninayofuata;

atakapomaliza kunipima

nitatoka mule safi kama zahabu.

11Ninamufuata kabisa;

njia yake nimeishikilia wala sikugeuka pembeni.

12Sijaacha hata kidogo kushika amri yake;

maneno yake nimeyatunza ndani ya moyo wangu.

13Lakini yeye habadiliki, nani anayeweza kumugeuza?

Kitu anachotaka, ndicho anachofanya!

14Anatimiza yote aliyonipangia;

na mengi kama hayo yako katika akili yake.

15Kwa hivyo, ninatetemeka kwa hofu mbele yake;

hata nikifikiri tu ninapatwa na woga.

16Mungu amefanya moyo wangu uregee,

Mungu Mwenye Uwezo amenitia hofu.

17Maana nimepatwa na giza,

na giza kubwa limetanda katika uso wangu.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help