Zaburi 57 - Swahili Congo Revised Bible 2002

Kuomba musaada

1Kwa mukubwa wa waimbaji. Kwa mutindo wa wimbo “Usiharibu.” Mashairi ya Daudi alipomuponyoka Saulo na kujificha katika pango.

2Unihurumie, ee Mungu, unihurumie,

maana ninakukimbilia wewe.

Ninakimbilia kwenye kivuli cha mabawa yako,

mpaka zoruba ya maangamizi ipite.

3Ninamulilia Mungu Mukubwa,

Mungu anayenikamilishia nia yake.

4Atanipelekea musaada toka mbinguni na kuniokoa,

atawafezehesha hao wanaonishambulia.

Mungu atanionyesha wema na uaminifu wake!

5Mimi nimezungukwa na waadui,

wenye uchu wa damu kama simba;

meno yao ni kama mikuki na mishale,

ndimi zao ni kama panga kali.

6Utukuzwe, ee Mungu, juu katika mbingu!

Utukufu wako uenee katika dunia yote!

7Waadui wamenitegea wavu waninase,

nami ninaugua kwa huzuni.

Wamenichimbia shimo katika njia yangu,

lakini wao wenyewe wametumbukia humo.

8Moyo wangu ni tayari, ee Mungu,

moyo wangu ni tayari;

nitaimba na kukushangilia!

9Amuka, ee nafsi yangu!

Muamuke, enyi kinubi na zeze!

Nitayaamusha mapambazuko!

10Ee Bwana, nitakushukuru kati ya watu;

nitakuimbia sifa kati ya mataifa.

11Wema wako unaenea hata juu katika mbingu,

uaminifu wako unafika hata katika mawingu.

12Utukuzwe, ee Mungu, juu katika mbingu!

Utukufu wako uenee katika dunia yote!

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help