Zaburi 23 - Swahili Congo Revised Bible 2002

Mungu ni muchungaji wangu

1Zaburi ya Daudi.

Yawe ni muchungaji wangu;

sitapungukiwa na kitu.

2Ananipumzisha kwenye majani mabichi;

ananiongoza kando ya maji matulivu,

3na kuirudishia nafsi yangu nguvu mupya.

Ananiongoza katika njia sawa

kwa utukufu wa jina lake.

4Hata nikipita katika bonde la giza kubwa,

sitaogopa hatari yoyote,

maana wewe, ee Yawe, ni pamoja nami;

gongo lako na fimbo yako vinanipa moyo.

5Umenitayarishia karamu mbele ya waadui zangu.

Umekipakaa kichwa changu mafuta.

Kikombe changu umekijaza tele.

6Kweli, uzuri na wema wako vitakuwa pamoja nami

siku zote za maisha yangu;

nami nitakaa katika nyumba ya Yawe milele.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help