Zaburi 50 - Swahili Congo Revised Bible 2002

Ibada ya kweli

1Zaburi ya Asafu.

Mungu, Mungu Yawe, amesema,

amewaita wakaaji wa dunia,

tokea magaribi mpaka mashariki.

2Kutoka Sayuni, muji muzuri kupita kipimo,

Mungu anajitokeza, akiangaza.

3Mungu wetu anakuja, lakini si kimyakimya:

moto wenye kuteketeza unamutangulia,

na zoruba kali inamuzunguka.

4Kutoka juu anaita mbingu na dunia

kuwa washuhuda wake atakapowahukumu watu wake.

5Yeye anasema:

“Munikusanyie waaminifu wangu,

waliofanya agano nami kwa njia ya sadaka!”

6Mbingu zinatangaza haki ya Mungu;

Mungu mwenyewe ndiye mwamuzi.

7“Enyi watu wangu, munisikilize,

mimi Mungu, Mungu wenu!

Ninataka kusema nanyi.

Israeli, ninakuonya.

8Sikukaripii kwa sababu ya sadaka zako;

haujaacha kunitolea sadaka za kuteketezwa.

9Kwa kweli sihitaji ngombe dume wa zizi lako,

wala beberu wa nyumba yako,

10maana nyama wote wa pori ni mali yangu,

na maelfu ya nyama wa milima ni wangu.

11Ndege wote wa mwitu ni mali yangu,

na viumbe vyote vinavyoishi katika pori ni vyangu.

12Kama ningesikia njaa, singekuambia wewe,

maana ulimwengu na vyote vinavyokuwa ndani yake ni vyangu.

13Unazani ninakula nyama ya ngombe dume,

au kunywa damu ya mbuzi?

14Shukrani ikuwe ndiyo sadaka yako kwa Mungu.

Umutimizie Mungu Mukubwa ahadi zako.

15Uniite wakati wa taabu,

nami nitakuokoa, nawe utanitukuza.”

16Lakini Mungu anamwambia mutu mwovu:

“Kwa nini kutajataja tu masharti yangu?

Kwa nini unasemasema juu ya agano langu?

17Wewe unachukia maonyo,

na maneno yangu haupendi kuyafuata.

18Ukimwona mwizi, unajiunga naye,

nawe unashirikiana na washerati.

19Uko tayari siku zote kusema mabaya;

kazi ya ulimi wako ni kutunga uongo.

20Unaikaa kitako kumuteta mwanadamu mwenzako,

unamuchongea ndugu yako wa tumbo.

21Umefanya hayo yote nami nimenyamaza.

Unazani kwamba mimi ni kama wewe?

Lakini sasa nitakukaripia,

nitakugombeza waziwazi.

22“Mufikiri vizuri jambo hili, enyi musionijali,

kama sivyo nitawaangamiza,

wala hakuna atakayewaokoa.

23Anayenitolea shukrani kama sadaka yake,

huyo ndiye anayenitukuza;

yeyote anayedumu katika njia yangu,

huyo ndiye nitakayemwokoa.”

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help