1Benjamina alizaa wana hawa: Bela, muzaliwa wake wa kwanza; Asibeli, wa pili; Ahara, wa tatu;
2Noha, wa ine; na Rafa, wa tano.
3Wana wa Bela walikuwa: Adari, Gera, Abihudi,
4Abisua, Namani, Ahoa,
5Gera, Sefufanu na Huramu.
6Hawa ndio wazao wa Ehudu waliokuwa viongozi wa jamaa za wale waliokuwa wakiishi Geba, lakini wakapelekwa katika uhamisho kule Manahati:
7Namani, Ahiya na Gera. Gera, baba ya Uza na Ahihudi, ndiye aliyewaongoza walipohamishwa.
8Saharaimu alizaa watoto katika inchi ya Moabu, nyuma ya kufukuza wanawake wake Husimu na Bara.
9Kisha aliishi katika inchi ya Moabu, akamwoa Hodesi, naye akamuzalia wana hawa: Yoabu, Sibia, Mesa, Malakamu,
10Yeusi, Sakia, na Mirma. Hawa wana wake wote walikuja kuwa wakubwa wa ukoo.
11Husimu muke wa Saharaimu alimuzaliwa wana wengine wawili: Abitubu na Elipali.
12Wana wa Elipali walikuwa: Eberi, Misamu na Semedi ambaye alijenga miji ya Ono na Lodi, pamoja na vijiji kandokando yake;
13Beria na Sema walikuwa kati ya jamaa ambazo zilikuwa zinaishi katika muji wa Ayaloni, na kuwafukuza wenyeji wa Gati. Wana wa Beria walikuwa:
14Ahio, Sasaki, Yeremoti,
15Zebadia, Aradi, Ederi,
16Mikaeli, Isipa na Yoa.
17-18Wana wa Epali walikuwa: Zebadia, Mesulamu, Hezekia, Heberi, Isinerai, Isilia na Yobabu.
19-21Wana wa Simei walikuwa: Yakimu, Sikiri, Zabudi, Elienai, Siletai, Elieli, Adaya, Beraya na Simuriti.
22-25Wana wa Sasaki walikuwa: Isipani, Eberi, Elieli, Abudoni, Sikiri, Hanani, Hanania, Elamu, Anetotiya, Ifedeya na Penueli.
26-27Wana wa Yohamu walikuwa: Samuserai, Seharia, Atalia, Yaresia, Elia na Sikiri.
28Hao ndio waliokuwa wakubwa wa ukoo zao kulingana na vizazi vyao. Walikuwa wanaishi Yerusalema.
29Yeieli alikuwa mwanzilishi wa muji wa Gibeoni. Muke wake aliitwa Maka.
30Muzaliwa wake wa kwanza alikuwa: Abudoni. Wana wake wengine walikuwa: Zuri, Kisi, Bali, Nadabu,
31Gedori, Ahio, Zekeri,
32na Mikiloti baba ya Simea. Hawa vilevile waliishi Yerusalema karibu na watu wengine wa ukoo wao.
Ukoo wa mufalme Saulo33Neri alizaa Kisi,
Kisi alizaa Saulo.
Saulo alizaa: Yonatani, Malkisua, Abinadabu na Esibali.
34Mwana wa Yonatani alikuwa: Meribu-Bali; Meribu-Bali alizaa Mika.
35Wana wa Mika walikuwa: Pitoni, Meleki, Terea na Ahazi.
36Ahazi alizaa Yera. Naye Yera alizaa Alemeti, Azimaweti na Zimuri. Zimuri alizaa Moza.
37Moza alizaa Binea, Binea alizaa Rafa, aliyemuzaa Eleasa, naye Eleasa alizaa Azeli.
38Wana wa Azeli walikuwa: Azirikamu, Bokeru, Isimaeli, Searia, Obadia na Hanani. Wote hao walikuwa wana wa Azeli.
39Nao wana wa ndugu yake Eseki walikuwa: Ulamu, muzaliwa wake wa kwanza; Yeusi, wa pili; na Elifeleti wa tatu.
40Wana wa Ulamu walikuwa watu mashujaa sana wa vita, na wapiga upinde hodari. Alikuwa na wana na wajukuu wengi, jumla yao walikuwa mia moja makumi tano. Hao wote waliotajwa hapo juu walikuwa wa ukoo wa Benjamina.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.