1Ninakimbilia kwako, ee Yawe,
usiniachilie kufezeheka hata kidogo!
2Kwa haki yako uniokoe na kunikomboa;
unitegee sikio lako na kuniokoa!
3Ukuwe kikingio changu cha kukimbilia,
kimbilio lenye nguvu la kuniokoa,
kwa maana wewe ni kikingio na kimbilio langu.
4Uniokoe, ee Mungu wangu, kutoka mikono ya waovu,
kutoka makucha ya watu wabaya na wakali.
5Maana wewe, Bwana wangu Yawe, ni tumaini langu,
tegemeo langu tangu ujana wangu.
6Nimekutegemea tangu kuzaliwa kwangu;
wewe ulinilinda nilipotoka katika tumbo la mama yangu.
Nitakusifu siku zote.
7Kwa wengi nimekuwa mushangao,
lakini wewe ni kimbilio langu lenye nguvu.
8Kinywa changu kimejaa sifa zako,
na utukufu wako muchana kutwa.
9Wakati wa uzee usinitupe;
ninapoishiwa na nguvu usiniachilie.
10Maana waadui zangu wanasema vibaya juu yangu;
wanaovizia maisha yangu wanafanya mipango,
11na kusema: “Mungu amemwachilia;
mumufuate na kumukamata,
kwa maana hakuna wa kumwokoa!”
12Usikae mbali nami, ee Mungu;
ukuje haraka unisaidie, ee Mungu wangu.
13Wapinzani wangu wote wafezeheke na kuangamizwa;
wenye kuvizia kuniua wafezeheke na kuzarauliwa.
14Lakini mimi nitakuwa na matumaini siku zote;
tena nitakusifu zaidi na zaidi.
15Kinywa changu kitaeleza matendo yako ya haki,
nitatangaza muchana kutwa matendo yako ya wokovu
ijapokuwa hayo yanapita akili yangu.
16Nitataja matendo yako makubwa, ee Bwana wangu Yawe;
nitatangaza kwamba wewe ndiwe mwenye haki.
17Ee Mungu, wewe umenifundisha tangu ujana wangu;
tena na tena, ninatangaza matendo yako ya ajabu.
18Usiniachilie, ee Mungu, nitakapokuwa muzee mwenye imvi nyingi,
kusudi nivitangazie vizazi vitakavyokuja nguvu yako.
19Nguvu na haki yako, ee Mungu,
vinafika mpaka juu katika mbingu.
Wewe umefanya mambo makubwa sana.
Ee Mungu, ni nani anayekuwa kama wewe?
20Umeniletea taabu kubwa,
lakini utanirudishia tena uzima,
wewe utaniinua tena kutoka katika shimo.
21Utaniongezea heshima yangu,
na kunifariji tena.
22Nami nitakusifu kwa kinubi,
kwa sababu ya uaminifu wako, ee Mungu wangu;
nitakuimbia sifa kwa zeze, ewe Mutakatifu wa Israeli.
23Nitanyanyua sauti kwa furaha,
ninapokuimbia wewe sifa zako,
na roho yangu itakusifu, maana umeniokoa.
24Nitatangaza haki yako muchana kutwa,
maana wanaonitakia hasara wamefezeheka na kuzarauliwa.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.