1Kwa mukubwa wa waimbaji. Zaburi ya Daudi.
Ee Yawe, wewe umenichunguza,
wewe unanijua mpaka ndani.
2Nikiikaa au nikisimama, wewe unajua;
wewe unajua kila kitu ninachofikiri juu yake.
3Nikienda au nikipumzika, unatambua;
wewe unajua shuguli zangu zote.
4Mbele sijasema neno lolote,
wewe, ee Yawe, unalijua kabisa.
5Uko kila upande wangu, mbele na nyuma;
unaniwekea mukono wako kwa kunilinda.
6Ufahamu wako unapita akili yangu;
ni mukubwa sana, siwezi kuuelewa.
7Nikimbilie wapi ambako roho yako haiko?
Niende wapi ambako wewe hauko?
8Nikipanda juu mbinguni, wewe ni kule;
nikijilaza chini katika kuzimu, wewe ni kule.
9Nikiruka mpaka mbali sana upande wa mashariki,
au hata kwa miisho upande wa magaribi,
10wewe uko hata kule kwa kuniongoza;
mukono wako wa kuume utanilinda.
11Kama ningeliomba giza linifunike,
giza linizunguke pahali pa mwangaza,
12kwako giza si giza hata kidogo,
na usiku unaangaa kama muchana;
kwako giza na mwangaza ni sawa.
13Wewe uliniumba mwili wangu wote;
ulinitengeneza katika tumbo la mama yangu.
14Ninakusifu maana umeniumba kwa namna ya ajabu.
Matendo yako ni ya ajabu.
Wewe unanijua kabisa kabisa.
15Umbo langu halikufichikwa kwako
nilipoumbwa kwa uficho,
nilipotengenezwa ndani ya tumbo la mama yangu.
16Wewe uliniona hata mbele sijazaliwa.
Uliandika kila kitu katika kitabu chako;
siku zangu zote ulizipanga,
hata mbele hakujakuwa ile ya kwanza.
17Ee Mungu, mawazo yako ni makubwa sana;
hayawezi kabisa kuhesabiwa.
18Ningeyahesabu yangekuwa mengi kuliko muchanga.
Hata ninapoamuka, ningali pamoja nawe.
19Heri, ee Mungu, ungewaua watu waovu!
Heri wauaji wangeniondokea!
20Wanasema vibaya juu yako;
wanasema maovu juu ya jina lako!
21Ee Yawe, ninawachukia wanaokuchukia;
ninawazarau sana wale wanaokuasi!
22Waadui zako ni waadui zangu;
ninawachukia kabisa kabisa.
23Unichunguze, ee Mungu, unijue moyo wangu,
unipime, uyajue mawazo yangu.
24Uangalie kama mwenendo wangu ni mubaya,
uniongoze katika njia ya milele.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.