1Kwa mukubwa wa waimbaji. Kwa filimbi. Zaburi ya Daudi.
2Ee Yawe,
usikilize maneno yangu,
usikie malalamiko yangu.
3Usikilize kilio changu,
Mufalme wangu na Mungu wangu,
maana wewe ndiwe ninayekuomba.
4Ee Yawe, kwa mapambazuko unasikia sauti yangu,
asubui ninakutolea sadaka yangu,
kisha ninangojea unijibu.
5Wewe si Mungu anayependa ubaya;
mwovu hawezi kupokelewa kwako.
6Wewe haupendi kuwaona wenye majivuno;
wewe unawachukia wote wanaotenda maovu.
7Unawaangamiza wote wanaosema uongo;
unawachukia wauaji na wadanganyifu.
8Lakini, kwa wingi wa wema wako,
mimi nitaingia ndani ya nyumba yako;
nitainama kwa heshima
kuelekea hekalu lako takatifu.
9Ee Yawe, katika haki yako,
uisawanishe njia yako mbele yangu.
Uniongoze kwa sababu ya waadui zangu.
10Ndani ya vinywa vyao hamuna ukweli wowote;
mioyo yao imejaa maangamizi,
koo zao ni kama kaburi wazi,
ndimi zao zimejaa udanganyifu.
11Ee Mungu, uwaazibu kwa makosa yao,
waanguke katika mipango yao wenyewe;
uwafukuze inje kwa sababu ya zambi zao nyingi,
kwa sababu wamekuasi wewe.
12Lakini wanaokimbilia kwako wafurahi wote,
waimbe kwa shangwe siku zote.
Uwalinde wanaolipenda jina lako,
kusudi wapate kushangilia kwa sababu yako.
13Maana wewe Yawe unawabariki watu wa haki;
unawakinga kwa upendo wako kama kwa ngao.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.