Ufunuo 19 - Swahili Roehl Bible 1937

Ndoa ya Mwana kondoo.

1Kisha nikasikia uvumi mkuu kama wa makundi mengi ya watu waliomo mbinguni, wakisema:

Haleluya! Wokovu na utukufu na uwezo ni wa Mungu wetu,

2kwani hukumu zake ni za kweli na za wongofu.

Kwani amemhukumu yule mgoni mkuu wa kike aliyeiangamiza

nchi kwa ugoni wake, akamlipiza damu za watumwa

wake waliouawa na mkono wake yeye.

7Tushangilie na kupiga vigelegele

na kumtukuza yeye! Kwani ndoa ya Mwana kondoo

imefika, naye mkewe amejitengeneza,

8akapewa kuvaa nguo za bafta zing'aazo na kumetuka.

Maana hizi nguo za bafta ndio wongofu, watakatifu

waliopewa.Mpanda farasi mweupe.

11Kisha nikaziona mbingu, zikifunuka, nikaona farasi mweupe; mwenye kumpanda anaitwa mwelekevu na mkweli, maana huamua kwa wongofu wa kuupigia vita.Kushindwa kwao yule nyama na mfumbuaji wa uwongo.

17Kisha nikaona malaika mmoja aliyesimama katika jua na kupaza sauti kuu akiwaambia ndege wote warukao mbinguni kati: Njoni, mkusanyikie vyakula vingi vya Mungu,Ez. 39:4,17-20.

18mpate kula nyama za miili ya wafalme na nyama za miili ya wakuu na nyama za miili ya wanguvu na nyama za miili ya farasi na ya wale waliowapanda na nyama za miili yawaungwana na ya watumwa wote walio wadogo na wakubwa!

19Nikamwona yule nyama na wafalme wa nchini na vikosi vyao vikikusanyika, wampelekee vita yeye aliyempanda yule farasi na makundi yake.Ufu. 16:14,16; 17:12-14; 19:11.

20Ndipo, yule nyama alipokamatwa pamoja na mfumbuaji wa uwongo; ni yule aliyevifanya vielekezo mbele yake vya kuwapoteza navyo wale waliojitia chapa cha yule nyama nao waliokiangukia kinyago chake. Wakingali wa hai hao wawili wakatupwa ziwani mwenye moto uwakao kwa nguvu za viberitiberiti vilivyomo.Ufu. 13:1,11-17; 20:10; Dan. 7:10,26.

21Nao waliosalia wakauawa kwa upanga uliotoka kinywani mwake yeye aliyempanda yule farasi. Nao ndege wote wakashiba nyama za miili yao.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help