1Unilinde, Mungu! Kwani nimekukimbilia.
2Nimemwambia Bwana: Wewe u bwana wangu; hakuna nionacho kuwa chema kisichotoka kwako.Sh. 73:25.
3Nao watakatifu waliopo katika nchi nimewaambia: Hawa ndio wakuu wa kweli, ndio wanipendezao kabisa.
4Maumivu yao wakimbiliao mwingine yatakuwa mengi; sitavimimina vinywaji vyao vya tambiko, maana ni vyenye damu, wala majina yao sitayatia tena midomoni mwangu.
5Bwana ni fungu langu, nililolitwaa, tena ni kinyweo, nilichopewa; wewe unanishikizia niliyopatiwa nilipopigiwa kura;Omb. 3:24.
6kamba zake ziliponiangukia niligawiwa pazuri, hilo fungu, nililolitwaa, linapendezeka kweli.
7Nitamkuza Bwana aniongozaye, mafigo yangu hunionya hivyo hata usiku.Sh. 4:5; 17:3.
8*Bwana na anisimamie kila, nitakapokuwa, awe kuumeni kwangu, nisitikisike.
9Kwa hiyo moyo wangu hufurahi, nayo yaliyo utukufu wangu hushangilia, hata mwili wangu utatulia kwa kuwa na kingojeo.1 Mose 49:6.
10Kwani hutaiacha roho yangu, ipotee kuzimuni, wala hutamtoa akuchaye, apate kuoza kaburini.Tume. 2:25-32; 13:35-37.
11Unanitambulisha njia iendayo penye uzima, utanishibisha furaha zilizopo usoni pako; mkono wako wa kuume hutoa kale na kale yapendezayo.*
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.