Marko 15 - Swahili Roehl Bible 1937

Kuhukumiwa.(1: Mat. 27:1-2; Luk. 22:66; 23:1; Yoh. 18:28.)

1Asubuhi kulipokucha, papo hapo watambikaji wakuu wakala njama pamoja na wazee na waandishi nao wote wa baraza ya wakuu wote, wakamfunga Yesu, wakampeleka, wakamtia mikononi mwa Pilato.

(2-19: Mat. 27:11-30; Luk. 23:2-25; Yoh. 18:29-19:16.)

2Pilato alipomwuliza: Wewe ndiwe mfalme wa Wayuda? akamjibu akimwambia: Wewe unavyosema, ndivyo.

3Watambikaji wakuu walipomsuta mengi,

4Pilato akamwuliza tena: Hujibu neno? Tazama yote, wanayokusuta!

5Lakini Yesu hakujibu neno tena, ikawa, Pilato akastaajabu.

6Kwa desturi ya sikukuu huwafungulia mfungwa mmoja, waliyemtaka.

7Kulikuwako mtu, jina lake Baraba, alifungwa pamoja na watu waliofunga kondo na kuua watu.

8Watu wengi walipokwenda bomani kwa kutaka, kwanza awafanyie, kama alivyozoea,

9Pilato akawajibu akisema: Mwataka, niwafungulie mfalme wa Wayuda?

10Kwani alitambua, ya kuwa watambikaji wakuu walikuwa wamemtoa kwa wivu.

29Waliopita wakamtukana, wakavitingisha vichwa vyao wakisema: Wewe unayelivunja Jumba la Mungu na kulijenga tena kwa siku tatu,Kufa.

33Ilipokuwa saa sita, pakawa na giza katika nchi yote nzima mpaka saa tisa. Ilipokuwa saa tisa, Yesu akapaza sauti sana:

34Eli, Eli, lama sabaktani? Maana yake ni kwamba: Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?Sh. 22:2.

35Wengine wao waliosimama hapo walipoyasikia wakasema: Tazama, anamwita Elia!

36Mmoja akapiga mbio, akachovya mwani sikini, akautia katika utete, akamnywesha akisema: Acheni, tuone, kama Elia anakuja kumshusha!

37Kisha Yesu akatoa sauti kubwa, nayo pumzi ikamtoka.

38Ndipo, pazia la Jumbani mwa Mungu lilipopasuka toka juu mpaka chini, likawa vipande viwili.

39Lakini bwana askari aliyesimama hapo na kumwelekea alipoona, pumzi ilivyomtoka, akasema: Kweli, mtu huyu alikuwa Mwana wa Mungu.

40Palikuwako nao wanawake, walisimama mbali wakitazama. Kati yao walikuwapo Maria Magadalene na Maria, mama yao Yakobo mdogo na Yose, na Salome;Luk. 8:2-3.

41ndio waliomfuata na kumtumikia yeye, alipokuwa huko Galilea. Palikuwako nao wengine wengi walipanda pamoja naye kwenda Yerusalemu.

Kuzikwa.(42-47: Mat. 27:57-61; Luk. 23:50-55; Yoh. 19:38-42.)

42Ilipokwisha kuwa jioni, kwa sababu ilikuwa andalio, ndio siku ya kutangulia sikukuu,

43akaja Yosefu wa Arimatia aliyekuwa mkuu mwenye macheo; naye mwenyewe alikuwa akiungoja ufalme wa Mungu. Akajipa moyo, akaingia kwa Pilato, akataka kupewa mwili wa Yesu.

44Pilato akastaajabu aliposikia, ya kuwa amekwisha kufa, akamwita bwana askari, akamwuliza, kama amekwisha kufa.

45Alipotambulishwa na bwana askari akampa Yosefu mwili wake.

46Naye akanunua sanda, akamshusha msalabani, akamtia katika ile sanda, akamweka katika kaburi lililochongwa mwambani, akafingirisha jiwe mlangoni pa kaburi.

47Nao akina Maria Magadalene na Maria, mama yake Yose, wakatazama, alipowekwa.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help