Waroma 9 - Swahili Roehl Bible 1937

Waisiraeli wa kweli.

1Kristo anajua: nasema kweli, sisemi uwongo; hata moyo wangu unaoyajua hunishuhudia katika Roho takatifu,

2ya kuwa masikitiko yangu ni makubwa, nao uchungu haukomi moyoni mwangu.

3Kwa hiyo naliomba mara kwa mara, mimi mwenyewe niapizwe, niondolewe kwake Kristo, kama hivyo vingeweza kuwaponya ndugu zangu, ambao tulizaliwa nao kimtu.

6Lakini sisemi hivyo, kwamba Neno lake Mungu limetenguka. Kwani walio kizazi chake Isiraeli sio wote Waisiraeli.

19Labda utaniambia: Mbona hutukamia? Kwani yuko nani ayapingaye mapenzi yake?

20Mwenzangu, u mtu gani ukitaka kubishana na Mungu? Je? Kiko chombo kitakachomwambia muumbaji: Mbona umenifanya hivi?

26Itakuwa hapo, hao wanaoambiwa sasa: Ninyi ham ukoo wangu,

waambiwe: M wanawe Mungu aliye Mwenye uzima.

28Kwani Bwana ndiye atakayevimaliza,

atakapolitimiza Neno lake nchini kwa kulikata.

29Navyo ndivyo, Yesaya alivyosema kale:

Bwana Mwenye vikosi kama asingalitusazia uzao,

tungalikuwa kama Sodomu, tungalifanana na Gomora.

30Basi, tusemeje? Ni hivi: Wamizimu wasiofuata wongofu wamepata wongofu; ni wongofu ule unaopatikana kwa kumtegemea Mungu.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help