4 Mose 33 - Swahili Roehl Bible 1937

Makambi ya Waisiraeli.

1Hizi ndizo safari za wana wa Isiraeli, vikosi vyao vilipotoka katika nchi ya Misri, wakiongozwa na Mose na Haroni.

2Mose akaziandika hizo safari zao, kama walivyotoka na kuondoka kwa kuagizwa na Bwana, nayo haya ndiyo matuo yao, walipoondoka kwendelea katika safari zao:

3siku ya kumi na tano ya mwezi wa kwanza, ndiyo siku ya pili ya Pasaka, ndipo, wana wa Isiraeli walipoondoka Ramusesi machoni pao Wamisri wote kwa nguvu za mkono uliotoka juu.

5Wana wa Isiraeli walipoondoka Ramusesi wakapiga makambi Sukoti.Waisiraeli wanaagizwa kuwaangamiza Wakanaani.

50Bwana akamwambia Mose huko kwenye mbuga za Moabu ng'ambo ya huku ya Yordani, Yeriko ukiwa ng'ambo ya pili, kwamba:

51Sema na wana wa Isiraeli, uwaambie: Mtakapouvuka Yordani kuingia katika nchi ya Kanaani.

52sharti mwafukuze mbele yenu wenyeji wote wa nchi hiyo, kisha myaharibu mawe yao yote yenye machorochoro ya kuyaangukia, navyo vinyago vyao vyote vilivyoyeyushwa sharti mviharibu, napo pao pote pa kutambikia vilimani sharti mpabomoe.

53Kisha mtaichukua hiyo nchi, mkae huko, kwani nimewapa ninyi nchi hiyo, mwichukue, iwe yenu.

54Nayo nchi mtaigawanyia ndugu zenu kwa kupiga kura; ndugu walio wengi mwagawie fungu kubwa zaidi kuwa lao, nao walio wachache mwagawie fungu lililo dogo kidogo kuwa lao. Huko, kura itakakomwangukia kila mtu, kutakuwa kwake; sharti mgawiane mafungu yenu kwa mashina ya baba zao.4 Mose 26:55.

55Lakini msipowafukuza mbele yenu wenyeji wa nchi hiyo, basi, hao mtakaowasaza watakuwa miiba machoni penu na machomo mbavuni penu, wawasonge ninyi katika nchi, mtakayoikaa ninyi.Yos. 23:13.

56Mwisho utakuwa, niwafanyizie ninyi yaleyale, niliyoyawaza kuwafanyizia wao.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help