1Katika mwaka wa 12 wa Ahazi, mfalme wa Wayuda, Hosea, mwana wa Ela, akapata kuwa mfalme wa Waisiraeli mle Samaria miaka 9.Kabila la Wasamaria linatokea.
24Kisha mfalme wa Asuri akatoa watu mle Babeli na Kuta na Awa na Hamati na Sefarwaimu, akawakalisha katika miji ya Samaria mahali pao wana wa Isiraeli, wakaitwaa nchi ya Samaria, iwe yao, wakakaa katika miji yao.
25Ikawa, walipoanza kukaa huko, hawakumcha Bwana, naye Bwana akatuma simba kwao, wakaua watu wengine wengine.
26Ndipo, walipotuma kumwambia mfalme wa Asuri kwamba: Wamizimu, uliowahamisha na kuwakalisha katika miji ya Samaria, hawayajui yampasayo Mungu wa nchi hii, kwa sababu hii ametuma simba kwao, nao wakawaua, kwa kuwa hawajui yampasayo Mungu wa nchi hii.
27Mfalme wa Asuri akaagiza kwamba: Pelekeni huko mmoja wao watambikaji, mliowatoa huko na kuwahamisha! Na aende, akae huko na kuwafundisha yampasayo Mungu wa nchi hiyo.
28Ndipo, mmoja wao watambikaji, waliowatoa Samaria na kuwahamisha, alipokuja, akakaa Beteli, akawa akiwafundisha njia za kumcha Bwana.
29Lakini kila kabila moja wakajitengenezea miungu ya kwao, wakaiweka katika zile nyumba, Waisiraeli walizozijenga vilimani za kutambikia mle; kila kabila moja wakafanya hivyo katika miji yao, walimokaa.
30Watu wa Babeli wakatengeneza vinyago vya Sukoti-Benoti, watu wa Kuta wakatengeneza vinyago vya Nergali, watu wa Hamati wakatengeneza vinyago vya Asima,
31watu wa Awa wakatengeneza vinyago vya Nibuhazi na vya Tarkati, nao wa Sefarwaimu wakawateketeza wana wao motoni, wawe ng'ombe za tambiko za Adarameleki na za Anameleki, ndiyo miungu yao wa Sefarwaimu.2 Fal. 17:17.
32Basi, hivyo walikuwa wakimcha Bwana, lakini wakajipatia miongoni mwao watambikaji wa vilimani, ndio waliowafanyia kazi za kutambika katika nyumba za vilimani.
33Hivyo walikuwa wenye kumcha Bwana pamoja na kuitumikia miungu ya kwao, kama ilivyowapasa wamizimu wa kwao, walikotolewa na kuhamishwa kuja huku.
34Hata siku hii ya leo hufanya, kama hizo desturi zao za kwanza zilivyokuwa: hawamchi Bwana kwa kweli, wala hawafanyi kwa kweli, maongozi yao na desturi zao zilivyo, wala hawaishiki njia ya Maonyo na ya maagizo, Bwana aliyowaagiza wana wa Yakobo, aliyempa jina la Isiraeli.
35Naye Bwana alikuwa amefanya agano nao na kuwaagiza kwamba: Msiche miungu mingine, wala msiiangukie, wala msiitumikie, wala msiitambikie!2 Mose 23:24.
36Ila Bwana aliyewatoa katika nchi ya Misri kwa nguvu kuu za mkono wake, alioukunjua, yeye sharti mmche, mmwangukie na kumtambikia!
37Nayo maongozi na maamuzi na Maonyo na maagizo, aliyowaandikia ninyi, sharti myaangalie, myafanye siku zote! Msiche kabisa miungu mingine!
38Wala msilisahau Agano, nililolifanya nanyi, wala msiche miungu mingine!5 Mose 6:12-19.
39Ila Bwana Mungu wenu sharti mmche! Naye atawaponya mikononi mwa adui zenu wote.
40Lakini hawakusikia, ila wao wakafanya, kama hizo desturi zao za kwanza zilivyokuwa.
41Hivyo ndivyo, hao wamizimu walivyomcha Bwana pamoja na kuvitumikia vinyago vyao. Hata wana wao na wana wa wana wao wakayafanya mpaka siku hii ya leo, kama baba zao walivyoyafanya.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.