1Malaika wa tano alipopiga baragumu, nikaona nyota iliyokuwa imetoka mbinguni, ikaanguka nchini. Kisha ikapewa ufunguo wa kisima cha kuzimu,
12Pigo la kwanza limekwisha pita; tazama, yako bado mawili, yanakuja baadaye.Baragumu la sita.
13Malaika wa sita alipopiga baragumu, nikasikia sauti moja iliyotoka katika zile pembe nne za meza ya Bwana ya dhahabu iliyokuwako mbele ya Mungu,Ufu. 8:3; 2 Mose 30:1-3.
14ikamwambia yule malaika wa sita aliyekuwa na baragumu: Wafungue wale makaika wanne waliofungwa kwenye mto mkubwa wa Eufurati.Ufu. 16:12.
15Ndipo, walipofunguliwa wale malaika wanne waliokuwa wamewekewa saa hii ya siku hii ya mwezi huu wa mwaka huu, waliue fungu la tatu la watu.Ufu. 8:7-12.
16Hesabu ya vikosi vya wapanda farasi ilikuwa elfu ishirini mara elfu kumi (20000000); ndiyo hesabu yao, niliyoisikia.
17Nilipowatazama wale farasi nao waliowapanda, nikawaona kuwa hivyo: walikuwa wamevaa nguo za vyuma kama za moto, nyingine nyeusi, nyingine za manjano. Vichwa vya farasi vilikuwa kama vya simba, tena katika vinywa vyao hutoka moto na moshi na viberitiberiti.
18Fungu la tatu la watu likauawa kwa mapigo hayo matatu, kwa moto na kwa moshi na kwa viberitiberiti vilivyotoka vinywani mwao.
19Kwani nguvu za hao farasi zimo vinywani mwao namo mikiani mwao. Kwani mikia yao imefanana na nyoka wenye vichwa; hiyo ndiyo, waliyopotoa nayo.
20Watu waliosalia, wasiouawa na mapigo hayo, hawakuyajutia matendo ya mikono yao, maana hawakuacha kutambikia mizimu na vinyago vya dhahabu na vya fedha na vya shaba na vya mawe na vya miti visivyoweza kuona wala kusikia wala kwenda.Ufu. 16:9,11,21; 1 Kor. 10:20.
21Kwa hiyo hawakujutia wala uuaji wao wala uchawi wao wala ugoni wao wala wizi wao.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.