1Kora, mwana wa Isihari, mwana wa Kehati, mwana wa Lawi, akachukua watu, yeye na Datani na Abiramu, wana wa Eliabu, na Oni, mwana wa Peleti, waliokuwa wana wa Rubeni.Vyetezo vyao wenzake Kora navyo vya Haroni.
36Bwana akamwambia Mose kwamba:
37Mwambie Elazari, mwana wa mtambikaji Haroni, aviokote vyetezo hapo, wale walipoteketezwa, kwani ni vitakatifu; nayo makaa ya moto uyamwage huko na huko.
38Kisha hivyo vyetezo vya hao wakosaji waliojipatia kufa wenyewe vitengenezeni kuwa mabati mapana ya kuifunikiza meza ya kutambikia. Kwa kuwa walivitokeza mbele ya Bwana, ni vitakatifu, navyo sharti viwe kielekezo kwao wana wa Isiraeli.
39Naye mtambikaji Elazari akavichukua hivyo vyetezo vya shaba, wao walioteketea walivyovitokeza mbele ya Bwana, wakavisana, viwe kifuniko cha meza ya kutambikia.
40Hivyo vikawa ukumbusho wa wana wa Isiraeli, kwa kwamba mtu mgeni asiye wa uzao wa Haroni, asije kuvukiza mavukizo mbele ya Bwana, asipatwe na mambo kama Kora na wenzake, aliowakusanya, maana Bwana alivyomwambia kinywani mwa Mose yalimpata.
Mapatilizo yao walionung'unikia kufa kwao wa Kora.41Kesho yake wao wote wa mkutano wa wana wa Isiraeli wakamnung'unikia Mose na Haroni kwamba: Mmewaua watu wa Mungu.
42Ikawa, huo mkutano ulipokusanyika kutetana na Mose na Haroni, nao hao walipoligeukia Hema la Mkutano, mara lile wingu likalifunika, nao utukufu wa Bwana ukatokea.4 Mose 14:10.
43Mose na Haroni walipokwenda kufika hapo mbele ya Hema la Mkutano,
44Bwana akamwambia Mose kwamba:
45Jiepusheni katikati ya mkutano huu, niwamalize kwa mara moja! Ndipo, walipoanguka kifudifudi,4 Mose 16:4,22.
46naye Mose akamwambia Haroni: Chukua chetezo, utie humo moto wa mezani pa kutambikia, kisha weka mavukizo juu yake, uende upesi kwenye mkutano, uwapatie upozi, kwani makali yamekwisha kutoka kwake Bwana, nalo pigo limekwisha kuwaanzia.2 Mose 28:38; 3 Mose 16:13.
47Haroni akachukua chetezo, kama Mose alivyosema, akapiga mbio kufika katikati ya mkutano, akaona, ya kuwa pigo limeanza kweli kupiga watu; ndipo, alipotia mavukizo juu ya moto, awapatie watu upozi.
48Aliposimama katikati yao waliokufa nao walio wazima bado, hilo pigo likakomeshwa.
49Nao waliouawa na hilo pigo walikuwa watu 14700, wasipohesabiwa waliokufa kwa ajili ya Kora.
50Kisha Haroni akarudi kwa Mose hapo pa kuliingilia Hema la Mkutano, hilo pigo lilipokuwa limekomeshwa.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.