1 Mose 18 - Swahili Roehl Bible 1937

Mungu anamtokea Aburahamu tena.

1Kisha Bwana akamtokea katika kimwitu cha Mamure, mwenyewe alipokuwa amekaa hapo pa kuingia hemani kwa kuwa jua kali.

2Alipoyainua macho yake akaona watu watatu, wakisimama hapo, alipo; alipowaona akawapigia mbio na kuondoka hapo pa kuingia hemani, akawainamia chini,Aburahamu anawaombea Wasodomu

23Aburahamu akafika karibu, akauliza: Utamwondoa mwongofu pamoja naye asiyekucha?4 Mose 16:22; 2 Sam. 24:17.

24Labda mle mjini wamo waongofu 50; basi, utawaondoa nao? Hutapahurumia mahali hapo kwa ajili ya waongofu 50 waliopo?

25Jambo kama hilo halipasi kabisa, ulifanye, ukimwua mwongofu pamoja naye asiyekucha, mwongofu akiwa kwako kama mwingine asiyekucha. Hili halikupasi kabisa wewe utakayewaamua walimwengu wote, hayo si maamuzi, utakayoyaamua.

26Bwana akasema: Kama nitawaona waongofu 50 mle mjini mwa Sodomu, nitapahurumia mahali pale pote kwa ajili yao.Yes. 65:8; Ez. 22:30; Mat. 24:22.

27Aburahamu akajibu kwamba: Tazama nimejipa moyo wa kusema na Bwana, ingawa mimi ni mavumbi na majivu.

28Labda wale waongofu 50 wamepunguka watano, sasa utaungamiza mji wote kwa ajili ya hao watano? Akasema: Sitauangamiza, kama nitaona humo 45.

29Akaendelea kusema naye kwamba: Labda wataonekana humo 40 tu. Akasema: Sitafanya kitu kwa ajili yao hao 40.

30Akasema: Makali ya Bwana yasiwake moto, nikisema tena: Labda wataonekana humo 30 tu. Akasema: Sitafanya kitu, kama nitaona humo 30 tu.Amu. 6:39.

31Akasema: Tazama, nimejipa moyo wa kusema na Bwana: Labda wataonekana humo 20 tu. Akasema: Sitauangamiza kwa ajili yao hao 20.

32Akasema: Makali ya Bwana yasiwake moto, nikisema tena mara moja tu: Labda wataonekana humo 10 tu. Akasema: Sitauangamiza kwa ajili yao hao 10 tu.

33Bwana alipokwisha kusema na Aburahamu akaenda zake, naye Aburahamu akarudi mahali pake.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help