1Isiraeli alipokuwa kijana, nilimpenda; huko Misri ndiko, nilikomwitia mwanangu.
9Sitayafanya, ukali wangu wenye moto uyatakayo,
sitamwangamiza tena Efuraimu,
kwani mimi ni Mungu, si mtu;
namo katikati yenu mimi ni mtakatifu,
nisije kuingia kwenu kwa machafuko.
10Watakuja kumtafuta Bwana, atakaponguruma kama simba;
kweli atakaponguruma, ndipo, watakapokuja kwa kutetemeka
wao watoto watokao upande wa baharini.
11Watamkimbilia kama ndege kwa kutetemeka wakitoka Misri,
au kama hua wakiitoka nchi ya Asuri;
ndipo, nitakapowakalisha nyumbani mwao; ndivyo, asemavyo Bwana.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.