Luka 14 - Swahili Roehl Bible 1937

Mwenye safura.

1*Ikawa, alipoingia siku ya mapumziko nyumbani mwa mkuu wa Mafariseo, ale chakula, wakawa wakimtunduia.Vyakula vya wageni.

12Kisha akamwambia yule aliyemwalika: Unapofanya karamu ya mchana au ya jioni usiwaalike rafiki zako wala ndugu zako wala jamaa zako wala majirani walio wenye mali! Maana wasikualike tena, nawe ukapata kulipwa.

13Ila unapofanya karamu uwaalike wakiwa na wavilema na viwete na vipofu!Karamu kubwa.

15Mmoja wao walikaa pamoja naye chakulani alipoyasikia haya akamwambia: Mwenye shangwe ndiye atakayekula chakula katika ufalme wa Mungu.(16-24: Mat. 22:2-10.)

16*Naye akamwambia: Kulikuwa na mtu aliyetengeneza karamu kubwa, akaalika wengi.

17Saa ya karamu ilipotimia, akatuma mtumwa wake, aende, awaambie walioalikwa: Njoni! Kwani vyote viko tayari.

18Wakaanza wote pamoja kuja kujipuzapuza. Wa kwanza akamwambia: Nimenunua shamba, sina budi kwenda, nilitazame; nakuomba, usiniwekee mfundo!

19Mwingine akasema: Nimenunua ng'ombe kumi wa kuvuta magari, nami ninakwenda, niwajaribu; nakuomba, usiniwekee mfundo!

20Mwingine akasema: Nimeoa mke, kwa hiyo siwezi kuja.1 Kor. 7:33.

21Basi, mtumwa akarudi, akamsimulia bwana wake. Ndipo, yule mwenye nyumba alipochafuka, akamwambia mtumwa wake: Toka, uende upesi, ufike kwenye viwanja na njia za mjini, ulete wakiwa na wavilema na vipofu na viwete, uwaingize humu!

22Kisha mtumwa akasema: Bwana, imekwisha fanyika, uliyoniagiza, lakini hamjajaa bado.

23Naye bwana akamwambia mtumwa: Toka, ufike njiani na nyugoni, uwashurutishe kuingia, nyumba yangu ipate kujaa!

24Kwani nawaambiani: Waume wale waliokuwa wamealikwa hakuna hata mmoja wao atakayevionja vyakula vyangu.*

Kumfuata Yesu.(26-27: Mat. 10:37-38.)

25Walipofuatana naye makundi mengi, akageuka, akawaambia:

26Mtu akija kwangu asipomchukia baba yake na mama yake na mkewe na watoto wake na ndugu zake wa kiume na wa kike, hata asipoichukia roho yake mwenyewe, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.Luk. 18:29-30; 5 Mose 33:9-10.

27Naye asiyeuchukua msalaba wake na kunifuata hawezi kuwa mwanafunzi wangu.Luk. 9:23.

28Maana kwenu yuko mtu anayetaka kujenga mnara, asiyekaa kwanza na kuzihesabu shilingi za jengo, kama anazo za kulitimiza?

29Kwani akiisha kuweka msingi, asipoweza kumaliza, halafu wote wanaoviona wataanza kumfyoza

30wakisema: Mtu huyu alianza kujenga, naye hakuweza kumaliza.

31Au yuko mfalme anayekwenda vitani kushindana na mfalme mwenzake pasipo kukaa kwanza na kufikiri, kama ataweza kuwatuma askari wake elfu kumi, wakutane na yule anayemjia na askari elfu ishirini?

32Kama haviwezi, atatuma wajumbe, yule mwingine akingali mbali bado, amwombe mapatano.

33Vivyo hivyo hata kila mmoja wenu asiyeviacha vyote, alivyo navyo, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.

34Chumvi ni nzuri, lakini chumvi ikiwa imepotewa na ukolezi itatiwa kiungo gani, ipate kukolea tena?Mat. 5:13; Mar. 9:50.

35Haitafaa tena, wala kutupwa shambani wala penye mbolea, ile huitupa nje tu. Mwenye masikio yanayosikia na asikie!

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help