Zakaria 8 - Swahili Roehl Bible 1937

Wokovu wao walio ukoo wake Mungu.

1Neno la Bwana Mwenye vikosi likanijia la kwamba:

2Hivi ndivyo, Bwana Mwenye vikosi anavyosema: Nimeingiwa na wivu mwingi sana kwa ajili ya Sioni, wivu huu ukanitia makali mengi yenye moto kwa ajili yake.

18Neno la Bwana Mwenye vikosi likanijia la kwamba:

19Hivi ndivyo, Bwana Mwenye vikosi anavyosema: Mifungo ya mwezi wa nne na wa tano na wa saba na wa kumi itageuka kuwa siku za furaha na za shangwe kwao walio mlango wa Yuda, zitakuwa sikukuu zipendezazo. Lakini sharti myapende mambo ya kweli na matengemano!Zak. 7:3,5; Yer. 41:1; 52:4-6,12.

20Hivi ndivyo, Bwana Mwenye vikosi anavyosema: Yako makabila mazima ya watu watakaokuja pamoja na wenyeji wa miji mingi.

21Wenyeji wa mji mmoja watakwenda kwa wenyeji wa mji mwingine kuwaambia: Haya! Twende kujinyenyekeza mbele ya Bwana na kumtafuta Bwana Mwenye vikosi! Mimi nami nitakwenda.

22Ndipo, watakapokuja watu wa makabila mengi, hata wamizimu wenye nguvu, wakimtafuta Bwana Mwenye vikosi mle Yerusalemu, wajinyenyekeze mbele ya Bwana.

23Hivi ndivyo, Bwana Mwenye vikosi anavyosema: Siku hizo itakuwa, watu kumi waliotoka katika misemo yote ya wamizimu wamshike mtu mmoja wa Kiyuda wakikamata pindo la nguo yake, kisha watamwambia: Tunataka kwenda nanyi, kwani tumesikia, ya kuwa Mungu yuko pamoja nanyi.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help