Mashangilio 4 - Swahili Roehl Bible 1937

Wimbo wa jioni wa kumtegemea Mungu.Kwa mwimbishaji, wa kuimbia mazeze. Wimbo wa Dawidi.

1Ninapokulilia, niitikie, Mungu unipaye wongofu! Hunipatia mahali pakubwa, nikiwa nimesongwa; sasa nihurumie na kuyasikia maombo yangu!

2Ninyi wana wa watu mpendao mambo ya bure, mpaka lini mwanitia soni na kuninyima heshima, mpaka lini mtayanyatia yaliyo uwongo tu?

3Lakini tambueni, ya kuwa Bwana humkuza amchaye! Bwana hunisikia, kila ninapomlilia.

4Stukeni, msije kukosa! Semeni mioyoni mwenu, mnapolala, mpate kutulia!

6Wako wengi wanaosema kwamba: Yuko nani atakayetuonyesha kilicho chema? Bwana, utokeze mwanga wa uso wako, uwe juu yetu!

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help