1Lakini tulipokwisha kuagana nao tukatweka na kukielekeza chombo kwenda Ko kwa tanga moja; tulipofika, kesho yake tukaenda hapo Rodo; toka hapo tukafika Patara.
2Tukaona chombo cha kuvukia hata Ufoniki, tukajipakia humo, tukatweka.
3Tulipokuona kule Kipuro tukakuacha kushotoni, tukaendelea mpaka Ushami, tukashukia Tiro; kwani ndiko, chombo kilikoagiziwa kuipakua mizigo yake.
4Tulipowaona wanafuanzi tukakaa lhuko siku saba. Nao wakamwambia Paulo kwa nguvu ya Roho, asipande kwenda Yerusalemu.
27Siku zile saba ziliposalia kidogo kutimia, Wayuda walitoka Asia wakamwona Paulo hapo Patakatifu, wakalichanganya kundi lote la watu, wakamkamata kwa mikono yao,
28wakapiga kelele kwamba: Waume na Isiraeli, tusaidieni! Huyu ndiye yule mtu anayefundisha po pote watu wote, waubeze ukoo wetu nayo Maonyo, hata mahali hapa! Tena ameingiza Wagriki hapa Patakatifu, ndivyo, alivyopapatia uchafu mahali hapa Patakatifu.
37Walipotaka kumwingiza bomani, Paulo akamwambia mkuu wa askari: Niko na ruhusa kukuambia neno? Naye aliposema: Unajua Kigriki?
38Wewe si yule Mmisri aliyefanya kishindo siku hizi akichukua watu 4000 waliokuwa wauaji na kuwapeleka nyikani?
39Paulo akasema: Mimi ni mtu wa Kiyuda toka mji wa Tarso, ni mwenyeji wa mji huo wa Kilikia usio mdogo; nakuomba, nipe ruhusa ya kusema na watu.Tume. 9:11.
40Alipompa ruhusa, Paulo akasimama juu hapo pa kupandia, akawapungia watu mkono; nao walipokuwa kimya kabisa, akasema nao Kiebureo, akawaambia:
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.