Yosua 17 - Swahili Roehl Bible 1937

Fungu la nusu ya Manase.

1Kisha shina la Manase likapigiwa kura, kwani yeye alikuwa mwana wa kwanza wa Yosefu. Naye Manase mwanawe wa kwanza alikuwa Makiri, babake Gileadi; kwa kuwa huyu alikuwa mtu wa kupiga vita, alipewa Gileadi na Basani.

14Kisha wana wa Yosefu wakamwambia Yosua kwamba: Mbona umetupigia kura mara moja tu na kutupatia fungu moja tu, liwe letu, nasi tu watu wengi, kwa kuwa Bwana ametubariki mpaka sasa!

15Yosua akawaambia: Kama ninyi m watu wengi, haya pandeni kwenye misitu kuikata, mjipatie pa kukaa huko katika nchi ya Waperizi na katika nchi ya Majitu, ikiwa milima ya Efuraimu inawasonga, isiwatoshe.

16Ndipo, wana wa Yosefu waliposema: Milima hii haitutoshi kweli; lakini Wakanaani wote wanaokaa bondeni kwa Beti-Seani na katika vijiji vyake nao wanaokaa bondeni kwa Izireeli wako na magari ya chuma ya kupigia vita.

17Ndipo, Yosua alipowaambia wao wa mlango wa Yosefu, wao Wamanase na Waefuraimu, kwamba: Ninyi mkiwa watu wengi wenye nguvu kubwa, hamtapata kwa kura nchi moja tu, iwe yenu.

18Kwani nchi yote ya milima nayo ni yako; kweli ni yenye misitu, lakini huko ndiko, utakakoweza kujipatia pa kukaa wa kuikata, kwani mwisho, itakapotokea kuwa wazi, itakuwa yenu. Kwani Wakanaani mtawafukuza, ijapo wawe wenye magari ya chuma ya kupigia vita, tena ijapo nguvu zao zaidi.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help