1Hayo yalipokwisha, Dawidi akawapiga Wafilisti, akawashinda; kisha Dawidi akaishika mwenyewe hatamu ya mji mkuu, isishikwe tena na Wafilisti.
2Nao Wamoabu akawapiga, akawapima kwa kamba akiwalaza chini, akapima hivyo: wa kamba mbili wakawa wa kuuawa, nao wote wa kamba moja wakawa wa kuachwa uzimani; nao Wamoabu wakawa watumishi wa Dawidi, wakamletea mahongo.
3Kisha Dawidi akampiga Hadadezeri, mwana wa Rehobu, mfalme wa Soba, alipokwenda kuusimika tena ufalme wake huko kwenye jito la Furati.
4Dawidi akateka kwake wapanda farasi 1700 na askari waliokwenda kwa miguu 20000, nao farasi wote wa kuvuta magari Dawidi akawakata mishipa, akajisazia farasi wa magari mia tu.
15Dawidi akawa mfalme wa Waisiraeli wote, naye Dawidi akawatengenezea watu wake wote mashauri yaliyokuwa sawa, maana yaliongoka.
16Naye Yoabu, mwana wa Seruya, alikuwa mkuu wa vikosi, naye Yosafati, mwana wa Ahiludi, alikuwa mwandishi wa mambo yaliyopasa kukumbukwa.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.