Wagalatia 2 - Swahili Roehl Bible 1937

Paulo apatana na Petero na Yakobo na Yohana.

1Kisha miaka kumi na minne ilipopita, nikapanda tena kwenda Yerusalemu pamoja na Barnaba, nikamchukua naye Tito, aende pamoja nami.Kumwonya Petero.

11Lakini Kefa alipofika Antiokia, nikambishia usoni pake, kwani alichongewa.

12Maana kulikuwako waliotumwa na Yakobo; hao walipokuwa hawajaja bado, alikula pamoja na wamizimu. Lakini walipokuja, akatoweka na kujitenga, kwani aliwaogopa wale waliotahiriwa.Tume. 11:3.

13Nao wenzake wa Kiyuda waliokuwako wakaufuata huo ujanja wake, naye Barnaba akaponzwa na huo ujanja wao.

14Lakini nilipowaona, ya kuwa hawaishiki njia nyofu wakiifuata kweli ya Utume mwema, nikamwambia Kefa mbele yao wote: Wewe u Myuda; tena mwenendo wako ni wa kimizimu, sio wa Kiyuda; imekuwaje, wewe ukiwashurutisha wamizimu kufanya mwenendo wa Kiyuda?

15Sisi tumezaliwa kuwa Wayuda, hatu wakosaji waliotoka kwao wamizimu.

16Lakini twajua: mtu hapati wongofu akiyafanya Maonyo, ila hupata wongofu akimtegemea Kristo Yesu; nasi tukamtegemea Kristo Yesu, tupate wongofu kwa kumtegemea Kristo, siko kwa kuyafanya Maonyo. Kwani hakuna aliye wa kimtu atakayepata wongofu kwa kuyafanya Maonyo.Tume. 15:10-11; Rom. 3:20,28; 4:5; 11:6; Ef. 2:8.

17Lakini sisi tunaotaka kupata wongofu kwa kuwa wake Kristo, sasa wenyewe tukionekana kuwa wakosaji, je? Kristo naye siye mwenye kutumikia makosa? La, sivyo!

18Kwani nikiyajenga tena yale, niliyoyajengua, naonyesha, ya kama sipatani na mimi mwenyewe.

19Kwani hapo, niliposhindwa na Maonyo, ndipo, nilipoyafika Maonyo, nipate kumkalia Mungu, maana nimewambwa msalabani pamoja na Kristo.Rom. 7:6,11.

20Tena ninaishi, lakini sasa si mimi tena ninayeishi, ila Kristo ndiye anayeishi mwilini mwangu. Maana hivyo, ninavyoishi sasa mwilini, ninaishi kwa kumtegemea Mwana wake Mungu aliyenipenda, akajitoa kwa ajili yangu.Gal. 1:4; Yoh. 17:23.

21Gawio la Mungu silitangui. Kwani kama wongofu ungepatikana kwa kuyafanya Maonyo, basi, Kristo angekuwa amekufa bure.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help