4 Mose 20 - Swahili Roehl Bible 1937

Kufa kwake Miriamu.

1Mkutano wote wa wana wa Isiraeli walipofika katika nyika ya Sini katika mwezi wa kwanza, watu wakakaa Kadesi. Ndiko, Miriamu alikokufa; kisha akazikwa huko.Maji ya Magomvi.

2Wao wa mkutano wasipoona maji huko, wakamkusanyikia Mose na Haroni,Waedomu wanawakataza Waisiraeli kupita kwao.

14Kule Kadesi Mose akatuma wajumbe kwa mfalme wa Edomu kwamba: Hivi ndivyo, ndugu yako Isiraeli anavyosema: Wewe unayajua masumbuko yote yaliyotupata:1 Mose 32:8; Amu. 11:17; 5 Mose 23:7.

15baba zetu walishuka Misri, wakakaa huko siku nyingi, nao Wamisri wakatufanyizia mabaya sisi na baba zetu.

16Tulipomlilia Bwana, akatusikia, akatuma malaika, akatutoa Misri. Tazama, sisi tumo humo Kadesi, ndio mji wa mpakani kwenye nchi yako.2 Mose 23:20.

17Sasa tunataka kupita katika nchi yako, lakini hatutaki kupita mashambani wala mizabibuni, wala hatutakunywa maji ya visimani, ila tunataka kuishika njia ya mfalme tu, tusiiache kwenda kuumeni wala kushotoni, hata tuupite mpaka wako mwingine.4 Mose 21:22.

18Lakini Mwedomu akamwambia: Hutapita kwangu. Ila nitatoka mwenye upanga, nipigane na wewe.

19Wana wa Isiraeli wakamwambia: Tunataka kushika njia tu, tena tukinywa maji yako sisi na nyama wetu wa kufuga tutakulipa; hakuna jingine, tunalolitaka, ila kupita tu kwa miguu yetu.

20Lakini akasema: Huna ruhusa kupita. Kisha Waedomu wakatoka wenye watu wengi na wenye mikono ya nguvu, wawazuie.

21Ndivyo, Waedomu walivyowakataza Waisiraeli kupita mipakani kwao; ndipo, Waisiraeli walipogeuka, washike njia ya kupitia kando yao.

Kufa kwake Haroni.

22Kisha wana wa Isiraeli wakaondoka Kadesi, wakafika mkutano wao wote kwenye mlima wa Hori.

23Huko kwenye mlima wa Hori kwenye mipaka ya nchi ya Edomu Bwana akamwambia Mose na Haroni kwamba:

24Sasa Haroni atachukuliwa, awe pamoja nao walio wa ukoo wake, kwani hataingia katika nchi ile, nitakayowapa wana wa Isiraeli, kwa kuwa mlikibishia kinywa changu kwenye Maji ya Magomvi.

25Mchukue Haroni pamoja na mwanawe Elazari, uwapeleke mlimani kwa Hori juu.

26Huko umvue Haroni mavazi yake, umvike mwanawe Elazari! Kisha Haroni atachukuliwa, afe huko.3 Mose 21:10.

27Mose akafanya, kama Bwana alivyomwagiza, wakaupanda mlima wa Hori machoni pao wote walio wa mkutano.

28Kisha Mose akamvua Haroni mavazi yake, akamvika mwanawe Elazari; ndipo, Haroni alipokufa huko juu mlimani, kisha Mose na Elazari wakashuka mlimani.4 Mose 33:38; 5 Mose 10:6.

29Wote wa mkutano walipoona, ya kuwa Haroni amekwisha kufa, wakamwombolezea Haroni siku thelathini wao wote wa mlango wa Isiraeli.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help