1Bwana Mungu aliye Mungu kweli alisema, akaziita nchi, akianzia maawioni kwa jua, afike nako machweoni kwake.
16Lakini asiyemcha Mungu humwambia: Sababu gani unayasimulia maagizo yangu? Nacho kinywa chako kinayasemaje maneno ya Agano langu?Rom. 2:21-23.
17Nawe unachukizwa unapoonywa, nayo maneno yangu unayatupia nyuma.
18Ukiona mwizi, ni rafiki yako, tena hufanya bia nao walio wazinzi.Ef. 5:11.
19Kinywa chako unakisemesha yaliyo mabaya, ulimi wako hutunga madanganyo.
20Ukikaa na ndugu yako unamsengenya, naye mtoto wa mama yako unamtukana.
21Hivyo ndivyo, ulivyovifanya, nikavinyamazia; ndipo, uliponiwazia kuwa sawa kama wewe. Kwa hiyo ninakuonya nikivitolea machoni pako.Sh. 73:11.
22Nanyi mliomsahau Mungu, yatambueni, nisije kuwararueni, pasiwepo mponya!
23Kunishukuru ndio ng'ombe ya tambiko initukuzayo; hiyo ni njia ya kumwonyesha mtu wokovu wa Mungu.*
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.