1Kwa mapenzi yake Dario akaweka watawala nchi 120 wa kuuangalia ufalme, wakiwa po pote katika huo ufalme.
2Hao nao akawapatia wakuu watatu, mmoja wao akawa Danieli; wale watawala nchi hawakuwa na budi kuwatolea hawa hesabu, mfalme asipotelewe na mali.
3Ndipo, huyu Danieli alipowashinda wakuu wenziwe na watawala nchi, kwa kuwa Roho iliyo kuu ilikuwa mwake, naye mfalme akafikiri kumpa ufalme wote, auangalie.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.