Mashangilio 129 - Swahili Roehl Bible 1937

Masongano na wokovu wa Waisiraeli.Wimbo wa kupapandia Patakatifu.

1Wamenisonga mara nyingi tangu ujana wangu; ndivyo, watakavyosema wao Waisiraeli.

2Wamenisonga mara nyingi tangu ujana wangu, lakini hawakupata kunishinda.

3Walimaji walilima mgongoni kwangu, wakatengeneza kuko huko matuta mazima.

5Sharti watwezwe na kurudishwa nyuma wote wachukizwao na Sioni!

6Sharti wawe kama majani yaliyoko kipaani juu ya nyumba! Miche yao hunyauka ikiwa haijachanua bado.

7Hapo mvunaji hawezi kukijaza kiganja chake tu, wala mfunga miganda hapajazi penye kifua chake.

8Wapitao wasiseme: Bwana na awabariki! Lakini ninyi tunawabariki katika Jina la Bwana.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help