1Alipoingia tena katika nyumba ya kuombea, mle mlikuwa na mtu mwenye mkono uliokuwa umekaukiana.
2Wakamtunduia, kama atamponya siku ya mapumziko, wapate kumsuta.
3Akamwambia yule mwenye mkono uliokaukiana: Inuka, uje hapa katikati!
4Kisha akawauliza: Iko ruhusa siku ya mapumziko kufanya mema au kufanya maovu? kuponya roho ya mtu au kuiua? Waliponyamaza,
5ukali ukamjia, akawatazama waliokuwako, akausikitikia ugumu wa mioyo yao, akamwambia yule mtu: Unyoshe mkono wako! Alipounyosha, huo mkono wake ukageuka kuwa mzima.Kuponya watu wengi.(7-12: Mat. 12:15-16; Luk. 6:17-19.)
7Yesu akaondoka pamoja na wanafunzi wake kwenda upande wa baharini. Kundi la watu wengi sana waliotoka Galilea likamfuata. Tena wengi waliotoka Yudea
8na Yerusalemu na Idumea na ng'ambo ya Yordani na upande wa Tiro na Sidoni, wakamwendea, kwani waliyasikia yote, aliyoyafanya.Kuwachagua Mitume 12.(13-19: Mat. 10:1-4; Luk. 6:12-16.)
13Kisha akapanda mlimani, akawaita, aliowataka mwenyewe; wakaja kwake.
14Akawaweka kumi na wawili, wawe pamoja naye, apate kuwatuma kupiga mbiu,
15wakiisha kupewa nguvu za kufukuza pepo.
16Akawaweka hao kumi na wawili: Simoni akampa jina la Petero.(22-30: Mat. 12:24-32; Luk. 11:15-22; 12:10.)
22Nao waandishi waliokuwa wametelemka toka Yerusalemu walisema: Ana Belzebuli. Tena wakasema: Nguvu ya huyo mkuu wa pepo ndiyo, anayofukuzia pepo.
23Akawaita, akawaambia kwa mifano: Satani awezaje kumfukuza Satani mwenziwe?
24Ufalme unapogombana wao kwa wao, ufalme huo hausimamiki.
25Nayo nyumba inapogombana wao kwa wao, nyumba hiyo haitaweza kusimama.
26Naye Satani anapojiinukia mwenyewe na kujigombanisha hawezi kusimama, ila ataishiwa.
27Hakuna mtu awezaye kuingia katika nyumba ya mwenye nguvu, aviteke vyombo vyake, asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu; kisha ataweza kuiteka nyumba yake.
28Kweli nawaambiani: Wana wa watu wataondolewa yote, hata maneno yote ya kumbeza Mungu.
29Lakini mtu atakayembeza Roho Mtakatifu hapati kuondolewa kale na kale, ila kosa lake litamkalia pasipo mwisho.
30Aliwaambia hivyo kwa vile walivyosema: Ana pepo mchafu.Mama na ndugu.(31-35: Mat. 12:46-50; Luk. 8:19-21.)
31Kisha mama yake na ndugu zake wakaja, wakasimama nje, wakatuma mtu kwake, amwite.
32Kundi la watu likawamo likimzunguka, wakamwambia: Tazama, mama yako na ndugu zako wako nje, wanakutafuta.
33Akajibu akiwaambia: Aliye mama yangu ni nani? Ndugu zangu ni akina nani?
34Akawatazama waliokaa huko na huko, wakimzunguka pande zote, akasema: Watazameni walio mama yangu na ndugu zangu!
35Mtu ye yote atakayeyafanya, Mungu ayatakayo, huyo ndiye ndugu yangu na dada yangu na mama yangu.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.