1 Wakorinto 7 - Swahili Roehl Bible 1937

Unyumba.

1Mambo, mliyoniandikia, nayajibu hivi: Ni vizuri, mtu asipogusa mwanamke.

2Lakini kwa ajili ya ugoni kila mtu awe na mkewe mwenyewe, hata kila mwanamke awe na mumewe mwenyewe.

3Mume ampe mkewe yampasayo, naye mke ampe mumewe yayo hayo.

4Mke siye mwenye mwili wake, ila mumewe; vilevile naye mume siye mwenye mwili wake, ila mkewe.

5Msinyamane, isipokuwa mmepatana kukaa hivyo kitambo kidogo, mjipatie siku za kufunga na za kuomba. Kisha mwandamane tena, Satani asipate kuwajaribu, kwani hamwezi kuvumilia pasipo kukoma.

6Haya nayasema, kama ninavyoyatambua mimi, lakini siyo ya kuagiza.

7Kupenda napenda, watu wote wawepo kama mimi mwenyewe; lakini kila mtu amegawiwa na Mungu kipaji chake yeye, mmoja hivyo, mwenzake hivyo.Kuachana.

8Lakini wasiooa na wajane nawaambia: Itawafalia, wakikaa kama mimi.

9Lakini kama hawawezi kujivumiliza, na waoe. Kwani kuoa ndiko kuzuri kuliko kuchomwa na tamaa.

17Kwa hiyo nasema: Kila mtu avishike, Bwana alivyomgawia, kila mtu aendelee hivyo, alivyokuwa hapo, Mungu alipomwita! Hivyo ndivyo, ninavyoagiza katika wateule wote.Wanawali.

25Kwa ajili ya wanawali sikupata agizo la Bwana, ninawaambia, ninayoyatambua kwa hivyo, nilivyogawiwa na Bwana kuwa mwelekevu.

32Nataka, msipatwe na masumbuko. Asiyeoa huyasumbukia mambo ya Bwana, apate kumpendeza Bwana.

33Aliyeoa huyasumbukia mambo ya ulimwenguni, apate kumpendeza mkewe; hivyo amekwisha kugawanyika.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help