2 Wafalme 20 - Swahili Roehl Bible 1937

Kuugua na kupona kwake Hizikia.(Taz. Yes. 38:1-8; 2 Mambo 32:24-33.)

1Siku zile Hizikia akaugua, kufa kukamjia karibu. Ndipo, mfumbuaji Yesaya, mwana wa Amosi, alipokuja kwake, akamwambia: Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: yaliyo yako yaagizie walio wa mlango wako! Kwani wewe utakufa, hutarudi kuwa mzima tena.

2Akageuka na kuuelekeza uso wake ukutani, akamwomba Bwana kwamba:

3E Bwana, na uukumbuke mwenendo, nilioufanya mbele yako kwa welekevu, nikayafanya kwa moyo wote mzima yaliyo mema machoni pako. Kisha Hizikia akalia kilio kikubwa.

4Ikawa, Yesaya alipokuwa hajatokea mjini katikati, ndipo, neno la Bwana lilipomjia kwamba:

5Rudi kumwambia Hizikia aliye mkuu wao walio ukoo wangu: Hivi ndivyo, Bwana Mungu wa baba yako Dawidi anavyosema: Nimesikia kuomba kwako, nikayaona nayo machozi yako; na nikuponye, kesho kutwa upate kupanda kuingia Nyumbani mwa Bwana.

6Siku zako nitaziongeza na kukupa tena miaka kumi na mitano. Namo mkononi mwake mfalme wa Asuri nitakuponya, hata mji huu, maana nitaukingia mji huu kwa ajili yangu na kwa ajili ya mtumishi wangu Dawidi.Kufa kwake Hizikia.

20Mambo mengine ya Hizikia nayo matendo yake yote ya vitani yaliyokuwa yenye nguvu nayo, aliyoyafanya ya kutengeneza ziwa na mifereji ya kupeleka maji mjini, hayakuandikwa katika kitabu cha mambo ya siku za wafalme wa Wayuda?

21Hizikia alipokwenda kulala na baba zake, mwanawe Manase akawa mfalme mahali pake.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help