1Rehabeamu alipofika Yerusalemu, akaikusanya milango ya Yuda na ya Benyamini, watu 180000 waliochaguliwa kupiga vita, wapigane na Waisiraeli, wamrudishie Rehabeamu ufalme huo.
2Lakini neno la Bwana likamjia Semaya aliyekuwa mtu wa Mungu, kwamba:
3Mwambie Rehabeamu, mwana wa Salomo, mfalme wa Wayuda, nao Waisiraeli wote walioko katika nchi ya Yuda na ya Benyamini kwamba:
4Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Msipande kwenda kupigana na ndugu zenu! Rudini kila mtu nyumbani kwake! Kwani jambo hili limefanywa na mimi. Walipoyasikia maneno haya ya Bwana wakarudi wakiacha kumwendea Yeroboamu.
Miji ya Rehabeamu yenye maboma.5Rehabeamu alipokaa Yerusalemu akajenga miji yenye maboma katika nchi ya Yuda.
6Akajenga maboma Beti-Lehemu na Itamu na Tekoa,
7na Beti-Suri na Soko na Adulamu,
8na Gati na Maresa na Zifu,
9na Adoraimu na Lakisi na Azeka,
10na Sora na Ayaloni na Heburoni; hii ndiyo miji yenye maboma katika nchi ya Yuda na ya Benyamini.
11Haya maboma akayajenga kuwa yenye nguvu, akaweka humo wenye amri na vilimbiko vya vilaji na vya mafuta na vya mvinyo.
12Humo katika kila mji mmoja akaweka ngao na mikuki, akaijenga kuwa yenye nguvu nyingi mno. Nchi ya Yuda na ya Benyamini ikawa yake.
Watambikaji na Walawi wanamjia Rehabeamu.13Watambikaji na Walawi katika nchi zote za Isiraeli wakarudi upande wake na kutoka katika mipaka yao yote.
14Kwani Walawi wakayaacha malisho na mapato yao, wakaenda Uyuda na Yerusalemu, kwa kuwa Yeroboamu na wanawe waliwatupa, waiswe watambikaji wa Bwana.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.