1Nilipoyainua macho yangu tena, nichungulie, mara nikaona barua irukayo angani.
2Akaniuliza: Unaona nini? Nikasema: Mimi ninaona barua irukayo angani, urefu wake ni mikono ishirini, nao upana wake ni mikono kumi.
3Akaniambia: Hii ndio kiapizo kilichotika kuifikia nchi yote nzima, kwani kila mwizi ataondolewa huku, kama yalivyoandikwa upande wake mmoja, hata kila aapaye kiapo cha uwongo ataondolewa huku, kama yalivyoandikwa upande wake wa pili.
4Ndivyo, asemavyo Bwana Mwenye vikosi: Nimeitoa, ije kuingia nyumbani mwa mwizi namo nyumbani mwake aapaye kiapo cha uwongo na kulitaja Jina langu, nayo itatua katikati ya nyumbani mwake, hata iiangamize yote pamoja na miti yake na mawe yake.
Mwanamke ndani ya pishi kubwa.5Kisha malaika aliyesema na mimi akatoka, akaniambia: Yainue macho yako, uone, kama ndio nini litakalotokea.
6Nikauliza: Ndio nini? Akasema: Hili ndio pishi kubwa sana linalotokea. Tena akasema: Hili ndio mfano wa watu walioko katika nchi hii yote nzima.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.