Mashangilio 99 - Swahili Roehl Bible 1937

Kuushukuru utakatifu wa Mungu.

1Bwana ni mfalme, kwa hiyo makabila ya watu hutetemeka. Yeye anakaa juu ya Makerubi, lakini nchi inayumbayumba.

6Mose na Haroni walikuwa miongoni mwao watambikaji wake, Samueli alikuwa miongoni mwao waliolililia Jina lake.Yer. 15:1.

7Alisema nao akiwa amejificha katika wingu lililokuwa kama nguzo, wao wakayashika maneno, aliyowashuhudia, hata maagizo, aliyowapa.

8Bwana, wewe ndiwe Mungu wetu. uliwaitikia kwa kuwa Mungu wao aondoaye makosa, tena kwa ajili ya matendo yao ukawalipiza.

9Mtukuzeni Bwana, Mungu wetu! Mwangukieni mlimani kwenye utakatifu wake! Kwani Bwana Mungu wetu ni mtakatifu.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help