1Vivyo hivyo nanyi wake sharti mwatii waume wenu! Maana kama wako wasiolitii Neno, watatekwa kwa mwenendo wa wake zao pasipo kuambiwa maneno,Waume wawape wake zao macheo!
7Vilevile nanyi waume, mwendeleane na wake zenu na kuwatambua kuwa viumbe vinyonge kuliko ninyi! Tena waheshimuni! Maana nao watagawiwa urithi wao wa uzimani pamoja nanyi; fanyeni hivyo, msizuiliwe kuomba!
8*Kisha nyote mioyo yenu sharti iwe mmoja, mpate kuvumiliana na kupendana kama ndugu walio wenye uororo na unyenyekevu!
9Msimlipe mtu uovu kwa uovu, wala matukano kwa matukano! Ila wafanyao hivyo mwaombee mema! Kwani hayo ndiyo, mliyoitiwa, mwirithi mbaraka.
11Yaliyo mabaya ayaepuke, afanye mema,
atafute penye utengemano, apakimbilie!
12Maana macho ya Bwana huwatazama walio waongofu,
masikio yake huyasikia maombo yao.
Lakini uso wa Bwana huwapingia wafanyao mabaya.
Kristo alivyokwenda kuzimuni.13Yuko nani atakayewaponza ninyi, mkijikaza kufanya mema?
14Lakini ijapo mteswe kwa ajili ya wongofu mtakuwa wenye shangwe. Lakini msiyaogope maogopesho yao, wala msiyahangaikie!
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.