1Mashina yote ya Waisiraeli wakaja Heburoni kwake Dawidi, wakamwambia kwamba: Tazama, sisi na wewe tu mifupa ya mmoja, nazo nyama za miili yetu ni za mmoja.Dawidi anajijengea nyumba.(11-25: 1 Mambo 14:1-16.)
11Hiramu, mfalme wa Tiro, akatuma wajumbe kwa Dawidi na miti ya miangati na maseremala na waashi wa kujenga na mawe, wakamjengea Dawidi nyumba.
12Ndipo, Dawidi alipojua, ya kuwa Bwana amemweka kweli kuwa mfalme wao Waisiraeli, kwani ufalme wake ukaja kutukuka zaidi kwa ajili ya ukoo wake wa Waisiraeli.
Wakeze na wanawe Dawidi.13Kisha Dawidi akachukua tena masuria na wake mle Yerusalemu alipokwisha kuingia humo na kutoka Heburoni, Dawidi akazaa tena wana wa kiume na wa kike.
14Haya ndiyo majina ya wana, waliozaliwa mle Yerusalemu: Samua na Sobabu na Natani na Salomo,Luk. 3:31; Mat. 1:6.
15na Ibuhari na Elisua na Nefegi na Yafia,
16na Elisama na Eliada na Elifeleti.
Dawidi anawashinda Wafilisti.17Wafilisti waliposikia, ya kuwa wamempaka Dawidi mafuta, awe mfalme wa Waisiraeli, ndipo, Wafilisti wote walipopanda kumtafuta Dawidi. Dawidi alipovisikia, akashuka kuja ngomeni.
18Wafilisti wakaja, wakajieneza Bondeni kwa Majitu.
19Dawidi akamwuliza Bwana kwamba: Nikipanda kupigana na Wafilisti, utawatia mkononi mwangu? Bwana akamwambia Dawidi: Panda! Kwani nitawatia Wafilisti mkononi mwako.1 Sam. 30:8.
20Ndipo, Dawidi alipokuja Baali-Perasimu; Dawidi alipowapiga huko akasema: Bwana amewaatua adui zangu mbele yangu, kama maji yanavyoatua ukingo. Kwa sababu hii akapaita mahali pale jina lake Baali-Perasimu (Maatuko).
21Wakaacha kule vinyago vyao, lakini Dawidi na watu wake wakavichukua.
22Lakini Wafilisti wakapanda tena, wakajieneza kulekule Bondeni kwa Majitu.
23Naye Dawidi alipomwuliza Bwana, akamwambia: Usipande, ila uzunguke migongoni kwao, upate kuwajia ukitoka juu, misandarusi iliko.
24Hapo, utakaposikia vileleni kwa misandarusi shindo kama ya watu wapitao, basi, hapo piga mbio! Kwani ndipo, Bwana atakapotokea, akutangulie kuyapiga majeshi ya Wafilisti.
25Dawidi akafanya, kama Bwana alivyomwagiza, akawapiga Wafilisti toka Geba, hata mtu afike Gezeri.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.