Yosua 14 - Swahili Roehl Bible 1937
Nchi ya Kanaani inagawanywa.
1Hizi ndizo nchi, wana wa Isiraeli walizozipata katika nchi ya Kanaani kuwa mafungu yao; nao waliowagawanyia haya mafungu ni mtambikaji Elazari na Yosua, mwana wa Nuni, pamoja na wakuu wa baba za mashina ya wana wa Isiraeli.