Yohana 6 - Swahili Roehl Bible 1937

Kulisha watu 5000.(1-15: Mat. 14:13-21; Mar. 6:32-44; Luk. 9:10-17.)

1*Kisha Yesu akaondoka kwenda ng'ambo ya bahari ya Galilea iitwayo ya Tiberia.

2Kundi la watu wengi likamfuata, kwani waliviona vielekezo, alivyowafanyia wagonjwa.

3Yesu akapanda mlimani, akakaa huko pamoja na wanafunzi wake.

4Lakini Pasaka ilikuwa karibu, ndiyo sikukuu ya Wayuda.Yesu baharini.(16-21: Mat. 14:22-33; Mar. 6:45-52.)

16Lakini jua lilipokwisha kuchwa, wanafunzi wake wakatelemka kwenda baharini,

17wakaingia chomboni, wavuke kwenda Kapernaumu ng'ambo ya bahari. Giza ilipokwisha kuingia, Yesu alikuwa hajafika kwao bado.

18Namo baharini mkainuka mawimbi kwa upepo uliovuma na nguvu.

19Walipokwisha endelea mwendo wa nusu saa na kupita kidogo, wakamwona Yesu, anavyokwenda juu ya bahari na kukifikia chombo karibu, wakaogopa.

20Ndipo, alipowaambia: Ni miye, msiogope!

21Walipotaka kumwingiza chomboni, mara chombo kikawa ufukoni kwenye nchi, walikokwenda.

Mkate uliotoka mbinguni.

22Kesho yake kundi la watu waliosimama ng'ambo ya bahari waliona, ya kuwa hakuwako chombo kingine huko, ni kile kimoja tu. Nao walikuwa wameona, ya kuwa Yesu hakuingia chomboni pamoja na wanafunzi wake; waliona, wanafunzi wake walivyoondoka peke yao.

23Lakini vyombo vingine vilivyotoka Tiberia vikafika karibu ya mahali pale, walipokula mikate, Bwana akiiombea.

24*Watu walipoona, ya kuwa Yesu hayuko, ya kuwa wanafunzi wake hawako nao, wakaingia katika vile vyombo, wakafika Kapernaumu, wamtafute Yesu.

25Walipomwona ng'ambo ya bahari wakamwuliza: Mfunzi mkuu, umefika lini hapa?

26Yesu akawajibu akisema: Kweli kweli nawaambiani: Hamnitafuti, kwa maana mmeona vielekezo, ila kwa maana mmeila ile mikate, mkashiba.

27Sumbukieni vyakula! Lakini vile vinavyoangamia sivyo, ni vile vinavyokaa, viwafikishe penye uzima wa kale na kale, navyo ndivyo, Mwana wa mtu atakavyowapani ninyi. Kwani huyu ndiye, Baba Mungu aliyemwagiza hivyo na kumtia muhuri.

41Wayuda wakamnung'unikia, kwa sababu alisema: Mimi ndio mkate ulioshuka toka mbinguni,

42wakasema: Huyu siye Yesu, mwana wa Yosefu? Hatumjui baba yake na mama yake? Asemaje sasa: Nimeshuka toka mbinguni?

47*Kweli kweli nawaambiani: Anitegemeaye anao uzima wa kale na kale.Kuula mwili wa Mwana wa mtu.

52Wayuda wakabishana wao kwa wao wakisema: Huyu atawezaje kutupa mwili wake, tuule?

53Yesu akawaambia: Kweli kweli nawaambiani: Msipoula mwili wa Mwana wa mtu, tena msipoinywa damu yake, hamna uzima mwenu.

54Mwenye kuula mwili wangu na kuinywa damu yangu anao uzima wa kale na kale, nami nitamfufua siku ya mwisho.Kuungama kwake Petero.

66Tokea hapo wengi waliokuwa wanafunzi wake wakarudi nyuma, wasifuatane tena naye.

67Yesu alipowauliza wale kumi na wawili: Nanyi mwataka kujiendea?

68ndipo, Simoni Petero alipomjibu: Bwana, tumwendee nani? Wewe unayo maneno ya uzima wa kale na kale.Yoh. 6:63.

69Nasi tumekutegemea, tukatambua, ya kuwa wewe ndiwe Kristo, Mwana wake Mungu Mwenye uzima.*Yoh. 1:49; 11:27; Mat. 16:16.

70Yesu akawajibu: Mimi sikuwachagua ninyi kumi na wawili? Tena mmoja wenu ni msengenyaji!

71Hapo alimsema Yuda wa Simoni, yule Iskariota; kwani huyo ndiye aliyemchongea halafu. Naye alikuwa miongoni mwao wale kumi na wawili.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help