1Haleluya! Lishangilieni Jina lake Bwana! Mlio watumishi wake Bwana, shangilieni!
2Nanyi msimamao Nyumbani mwake Bwana, nanyi mlioko nyuani penye Nyumba ya Mungu wetu,
3mshangilieni Bwana! Kwani Bwana ni mwema. Liimbieni Jina lake na kupiga mazeze! Kwani ni zuri.
4Kwani Bwana alimchagua Yakobo, awe wake, yeye Isiraeli awe mali zake.
5Kwani mimi ninajua, ya kuwa Bwana ni mkuu, ya kuwa Bwana wetu anaipita miungu yote kwa huo ukuu.
13Bwana Jina lako ni la kale na kale, Bwana, ukumbuko wako ni wa vizazi na vizazi.(15-20: Sh. 115:4-11.)
15Vinyago vya wamizimu ni fedha na dhahabu, mikono ya watu ndiyo iliyovifanya:
16vinywa vinavyo, lakini havisemi, macho vinayo, lakini havioni,
17masikio vinayo, lakini havisikii; wala pumzi hazimo vinywani mwao.
18Kama hivyo vilivyo, ndivyo, watakavyokuwa nao waliovifanya; nao wote pia waviegemeao.
19Mlio wa mlango wa Isiraeli, mtukuzeni Bwana! Mlio wa mlango wa Haroni, mtukuzeni Bwana!Sh. 118:2-4.
20Mlio wa mlango wa Lawi, mtukuzeni Bwana! Mmwogopao Bwana, mtukuzeni Bwana!
21Bwana na atukuzwe mle Sioni, yeye akaaye Yerusalemu! Haleluya!
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.