Mashangilio 146 - Swahili Roehl Bible 1937

Kuutukuza msaada wa Mungu.

1Haleluya! Mshangilie Bwana, roho yangu!

2Na nimshangilie Bwana siku zangu za kuwapo! Na nimwimbie Mungu wangu na kupiga zeze nikingali nipo!

3Msiegemee wakuu! Nao ni wana wa watu, hawawezi kuokoa.

5Mwenye shangwe ni mtu wa Mungu wa Yakobo, maana humsaidia, akimngojea Bwana, Mungu wake.

6Yeye ndiye aliyezifanya mbingu na nchi, hata bahari navyo vyote vilivyomo. Yeye ndiye ashikaye welekevu na kuufuata kale na kale.

7Yeye ndiye anayewaamulia waliokorofishwa, yeye ndiye anayewashibisha wenye njaa.

Yeye Bwana ndiye anayewafungua waliofungwa,

8yeye Bwana ndiye anayefumbua macho ya vipofu, yeye Bwana ndiye anayewainua walioinamishwa, yeye Bwana ndiye anayewapenda waongofu,

10Bwana anashika ufalme kale na kale, Mungu wako, Sioni, ni wa vizazi na vizazi. Haleluya!

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help