1Nimeyainua macho yangu na kuyaelekeza kwako, ukaaye mbinguni.
2Kama macho ya watumishi yanavyoitazama mikono ya bwana zao, au kama macho ya mjakazi yanavyoitazama mikono ya bibi yake, hivyo macho yetu humtazama Bwana Mungu wetu, hata atuhurumie.
3Tuhurumie, Bwana! Tuhurumie! Kwani tumeshiba sana mabezo.
4Roho zetu zimeshiba sana masimango yao wanaokula vya urembo, nayo mabezo yao wenye majivuno.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.