Mashangilio 82 - Swahili Roehl Bible 1937

Mungu huwapatiliza waamuzi wabaya.Wimbo wa Asafu

1Mungu anasimama katika mkutano wao miungu mwingine, atoe hukumu katikati yao hiyo miungu.Sh. 82:6.

2Mpaka lini mtayapotoa maamuzi yenu mkiwa upande wao wasionicha?5 Mose 1:17.

3Waamulieni wakorofikao nao wafiwao na wazazi! Wanyonge na maskini watengenezeeni mashauri kwa wongofu!Yes. 1:17.

4Waopoeni wakorofikao nao wakiwa mkiwatoa mikononi mwao wasionicha!

5Lakini hawavitambui, wala hawaonyeki, ila hujiendea gizani, ijapo, shikizi zote za nchi zije kutikisika.

6Mimi nilisema: Ninyi m miungu, nyote m wanawe Alioko huko juu.Sh. 82:1; 2 Mose 21:6; Yoh. 10:34.

7Lakini mtakufa kweli kama wana wa watu, mtaanguka kama m wenzao walio wakuu.

8Inuka, Mungu! Ihukumu nchi! Kwani mwenye wamizimu wote ndiwe wewe.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help