1 Mambo 21 - Swahili Roehl Bible 1937

Dawidi anapatilizwa kwa kuwahesabu watu.(Taz. 2 Sam. 24.)

1Satani akawainukia Waisiraeli akimponza Dawidi, awahesabu Waisiraeli.

2Dawidi akamwambia Yoabu na wakuu wa watu: Nendeni, mwahesabu Waisiraeli toka Beri-Seba hata Dani! Kisha nileteeni habari, nipate kuzijua hesabu zao.

3Yoabu akamjibu: Bwana na aendelee kuwaongeza watu wake vivyo hivyo mara mia! Bwana wangu mfalme, kumbe wao wote sio watumishi wa bwana wangu? Hayo bwana wangu anayatakia nini? Kuwakosesha Waisiraeli hivyo ni kwa nini?

8Ndipo, Dawidi alipomwambia Mungu: Nimekosa sana kwa kulifanya neno hilo; sasa umwondolee mtumishi wako hizo manza, alizozikora! Kwani nimefanya kisichopasa kabisa.

9Lakini Bwana akamwambia Gadi aliyekuwa mchunguzaji wake Dawidi kwamba:

10Nenda kumwambia Dawidi kwamba: Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Mimi ninakuwekea mambo matatu, ndimo uchague moja lao, nikufanyizie.

11Gadi akaja kwa Dawidi, akamwambia: Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Jipatie ulitakalo!

12Unataka miaka mitatu ya njaa? au unataka kukimbizwa miezi mitatu machoni pao wakusongao, panga za adui zako zikikupata? au unataka, upanga wa Bwana na ugonjwa mbaya uuao upite katika nchi hii, malaika wa Bwana akifanya maovu katika mipaka yote ya Waisiraeli? Sasa tafuta, uone nitakayomjibu aliyenituma!

13Dawidi akamwambia Gadi: Nimesongeka sana, lakini na nijitupe mkononi mwake Bwana, kwani huruma zake ni nyingi mno nisijitupe mikononi mwa watu.

14Ndipo, Bwana alipowauguza Waisiraeli ugonjwa mbaya uuao, wakafa kwa Waisiraeli watu 70000.

15Mungu akamtuma malaika wake namo Yerusalemu, afanye humo namo maovu yake; lakini Bwana alipoyaona hayo maovu, aliyoyafanya, akageuza moyo kwa ajili ya huo ubaya, akamwambia yule malaika aliyeangamiza: Sasa inatosha, ulegeze mkono wako! Naye yule malaika wa Bwana alikuwa akisimama penye kupuria ngano pa Myebusi Ornani.

16Dawidi alipoyainua macho yake, akamwona malaika wa Bwana, akisimama kati ya nchi na ya mbingu, nao upanga uliochomolewa ulikuwa mkononi mwake kuuelekea Yerusalemu; ndipo, Dawidi na wazee waliokuwa wamevaa magunia walipoanguka kifudifudi,

17Dawidi akamwambia Mungu: Kumbe si mimi niliyeagiza kuwahesabu watu? Mimi ndiye niliyekosa na kufanya mabaya sana. Lakini hawa kondoo wamefanya nini? Bwana Mungu wangu, mkono wako na unipige mimi na mlango wa baba yangu! Lakini hawa walio ukoo wako usiwaue!

Dawidi anamtambikia Bwana penye kupuria ngano pa Ornani.

18Ndipo, malaika wa Bwana alipomwambia Gadi, amwambie Dawidi, Dawidi apande kutengeneza pa kumtambikia Bwana papo hapo penye kupuria ngano pa Myebusi Ornani.

19Kwa hilo neno, Gadi alilolisema katika Jina la Bwana, Dawidi akapanda.

20Ornani alipogeuka akamwona malaika; nao wanawe wanne waliokuwa naye walikuwa wamejificha, naye Ornani mwenyewe alikuwa akipura ngano.

21Dawidi alipokuja kwake Ornani, huyu Ornani alikuwa akitazama; alipomwona Dawidi, akatoka hapo pa kupuria ngano, akamwangukia Dawidi usoni hapo chini.

22Dawidi akamwambia Ornani: Nipe mahali hapa pa kupuria ngano, nipajenge pa kumtambikia Bwana! Nitakulipa fedha zote zipapasazo, nipe tu mahali hapa, huku kuuawa kwa watu kukomeshwe!

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help