Mashangilio 140 - Swahili Roehl Bible 1937

Kuomba wokovu kwenye watu wabaya.Kwa mwimbishaji. Wimbo wa Dawidi.

1Bwana, kwenye watu wabaya niopoe!

2nilinde, watu wenye makorofi wasinijie!

3Ndio wanaowaza mabaya mioyoni mwao, nao hufanya magomvi kila siku.

4Wamezinoa ndimi zao, ziwe kama za nyoka, sumu ya pili imo midomoni mwao.

5Niangalie, Bwana, mikono yao wasiokucha isinikamate! Nilinde, watu wenye makorofi wasinijie! Ndio wawazao, jinsi watakavyonikumba, nije kujikwaa

6Wenye majivuno wamenitegea matanzi na nyugwe, wakanitandikia nyavu kandokando ya njia, wakaiweka nayo mitego yao, waninase.

7Nikamwambia Bwana: Wewe ndiwe Mungu wangu! Bwana, zisikilize sauti za malalamiko yangu!

11Na awanyeshee mvua ya makaa ya moto! Na awakumbe, waanguke, motoni namo mashimoni, wasiweze kabisa kuinuka tena!

12Mtu mwenye masingizio hatashikizwa katika nchi, mtu mwenye makorofi mabaya na yamkimbize, mpaka aangamie!

13Ninajua, ya kuwa Bwana atamwamulia aliye mnyonge, nayo mashauri ya wakiwa atayanyosha.

14Watakaolishukuru Jina lako kweli ndio waongofu, nao wanyokao mioyo watakaa usoni pako.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help