2 Mose 17 - Swahili Roehl Bible 1937

Mose anatoa maji mwambani.

1Wao wote wa mkutano wa wana wa Isiraeli wakaondoka katika nyika ya sini kwenda safari zao kwa kuagizwa na Bwana, wakapiga makambi Refidimu, lakini maji ya kunywa watu hayakuwako.

2Ndipo, watu walipomgombeza Mose na kusema: Tupeni maji, tunywe! Mose akawaambia: Mbona mnanigombeza? Mbona mnamjaribu Bwana?Waamaleki wanashindwa.

8Waamaleki wakaja kupigana nao Waisiraeli huko Refidimu.4 Mose 13:8,16.

9Ndipo, Mose alipomwambia Yosua: Utuchagulie waume, utoke nao kupigana na Waamaleki! Mimi nami nitasimama kesho juu ya hiki kilima, nayo fimbo ya Mungu itakuwa mkononi mwangu.

10Yosua akafanya, kama Mose alivyomwagiza kwenda kupigana na Waamaleki, lakini Mose na Haroni na Huri wakakipanda hicho kilima, mpaka wafike juu.

11Ikawa, Mose alipouinua mkono wake, Waisiraeli wakashinda; lakini alipoushusha mkono wake, upumzike, Waamaleki wakashinda.

12Mikono ya Mose ilipolegea kwa kuwa mizito, wakachukua jiwe, wakaliweka chini yake, apate kulikalia. Kisha Haroni na Huri wakaishikiza mikono yake, mmoja huku, mmoja huko; ndivyo, mikono yake ilivyopata nguvu, mpaka jua lilipokuchwa,

13tena ndivyo, Yosua alivyowashinda Waamaleki na watu wao kwa ukali wa panga.

14Bwana akamwambia Mose: Yaandike haya katika kitabu, yakumbukwe siku zote! Tena mwelezee Yosua, ya kama nitafuta kabisa ukumbusho wote wa Waamaleki, watoweke chini ya mbingu.5 Mose 25:17-19; 1 Sam. 15:2-3.

15Kisha Mose akajenga pa kumtambikia Bwana, akapaita jina lake: Bwana ni Bendera yangu,

16kwani alisema: Bwana ameuweka mkono penye bendera kwamba: Bwana atapiga vita na Waamaleki kwa vizazi na vizazi.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help