Luka 20 - Swahili Roehl Bible 1937

Ubatizo wa Yohana.(1-8: Mat. 21:23-27; Mar. 11:27-33.)

1Ikawa siku moja, alipofundisha watu hapo Patakatifu na kuipiga hiyo mbiu njema, wakamwinukia watambikaji wakuu na waandishi na wazee,

2wakamwambia wakisema: Utuambie: Hayo unayafanya kwa nguvu gani? au ni nani aliyekupa nguvu hii?

3Akajibu akiwaambia: Hata mimi nitawauliza neno moja, mnijibu:

4Ubatizo wake Yohana ulitoka mbinguni au kwa watu?

5Wakafikiri mioyoni mwao kwamba: Tukisema: Ulitoka mbinguni, atatuuliza: Mbona hamkumtegemea?

6Lakini tukisema: Ulitoka kwa watu, watu wote watatupiga mawe. Kwani walikuwa wametambua kweli kwamba: Yohana ni mfumbuaji.

7Kwa hiyo wakajibu: Hatujui, ulikotoka.

8Ndipo, Yesu alipowaambia: Basi, hata mimi siwaambii nguvu inayonifanyisha hayo.

Wakulima wabaya.(9-19: Mat. 21:33-46; Mar. 12:1-12.)

9Akaanza kuwatolea watu mfano huu: Mtu alipanda mizabibu, akaipangisha wakulima, kisha akaenda katika nchi nyingine kukaa siku nyingi.

10Siku zilipotimia, akatuma mtumwa kwa wale wakulima, wampe matunda ya mizabibu. Lakini wakulima wakampiga, wakamrudisha mikono mitupu.

18Kila atakayeanguka juu ya jiwe lile atapondeka; naye litakayemwangukia, litambana tikitiki.

Shilingi ya kodi.

19Saa ileile waandishi na watambikaji wakuu wakatafuta kumkamata, lakini waliliogopa lile kundi la watu; kwani walitambua, ya kuwa amewasemea wao wenyewe mfano lhuo.(20-26: Mat. 22:15-22; Mar. 12:13-17.)

20Wakamtunduia, wakatuma wapelelezi, wafanye ujanja wa kuwa kama waongofu, maana wamnase kwa maneno yake, wapate kumpeleka bomani kwenye nguvu ya mtawala nchi.

43mpaka niwaweke adui zako chini miguuni pako!

44Basi, Dawidi akimwita Bwana, anakuwaje tena mwana wake?

Kujilinda kwa ajili ya waandishi.(45-47: Mat. 23:1, 5-7,14; Mar. 12:38-40.)

45Akawaambia wanafunzi, watu wote waliposikia:Luk. 11:43.

46Jilindeni kwa ajili ya waandishi wanaotaka kutembea wenye kanzu ndefu, tena hupenda kuamkiwa na watu sokoni! Namo nyumbani mwa kuombea hupenda viti vya mbele, hata wakialikwa chakulani hupenda kukaa penye wakuu.

47Huzila nyumba za wajane, wakijitendekeza, kama wanakaza kuwaombea. Walio hivyo mapatilizo yao yatakuwa kuliko ya wengine.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help