1Wana wa Lawi: Gersoni, Kehati na Merari.
16Wana wa Lawi: Gersomu, Kehati na Merari.
17Nayo haya ndiyo majina ya wana wa Gersomu: Libuni na Simei.
62Nao wana wa Gersomu walipewa miji 13, iwe ya ukoo wao katika shina la Isakari na katika shina la Aseri na katika shina la Nafutali na katika shina la Manase huko Basani.
63Nao wana wa Merari walipewa kwa kupigiwa kura miji 12, iwe ya ukoo wao katika shina la Rubeni na katika shina la Gadi na katika shina la Zebuluni.
64Ndivyo, wana wa Isiraeli walivyowapa Walawi hiyo miji pamoja na malisho yao.
65Wakawapa kwa kuipigia kura ile miji, iliyotajwa majina yao katika shina la wana wa Yuda na katika shina la wana wa Simeoni na katika shina la wana wa Benyamini.
66Nao wengine waliokuwa wa ukoo wa wana wa Kehati walipata miji katika shina la Efuraimu, iwe yao.
67Wakawapa miji ya kukimbilia ya Sikemu pamoja na malisho yake milimani kwa Efuraimu, tena Gezeri pamoja na malisho yake
68na Yokimamu pamoja na malisho yake na Beti-Horoni pamoja na malisho yake
69na Ayaloni pamoja na malisho yake na Gati-Rimoni pamoja na malisho yake.
70Tena katika nusu ya shina la Manase Aneri pamoja na malisho yake na Bileamu pamoja na malisho yake. Hii ilikuwa yao wengine wa ukoo wa wana wa Kehati waliosalia.
71Wana wa Gersomu walipata katika ukoo wao wa nusu ya shina la Manase Golani ulioko Basani pamoja na malisho yake na Astaroti pamoja na malisho yake.
72Tena katika shina la Isakari: Kedesi pamoja na malisho yake na Daberati pamoja na malisho yake
73na Ramoti pamoja na malisho yake na Anemu pamoja na malisho yake.
74Tena katika shina la Aseri: Masali pamoja na malisho yake na Abudoni pamoja na malisho yake
75na Hukoki pamoja na malisho yake na Rehobu pamoja na malisho yake.
76Tena katika shina la Nafutali: Kedesi wa Galili pamoja na malisho yake na Hamoni pamoja na malisho yake na Kiriataimu pamoja na malisho yake.
77Wana wa Merari waliosalia walipata katika shina la Zebuluni: Rimoni pamoja na malisho yake na Tabori pamoja na malisho yake;
78tena ng'ambo ya pili ya Yordani kuelekea Yeriko upande wa Yordani wa maawioni kwa jua katika shina la Rubeni: Beseri wa nyikani pamoja na malisho yake na Yasa pamoja na malisho yake
79na Kedemoti pamoja na malisho yake na Mefati pamoja na malisho yake.
80Tena katika shina la Gadi: Ramoti wa Gileadi pamoja na malisho yake na Mahanaimu pamoja na malisho yake
81na Hesiboni pamoja na malisho yake na Yazeri pamoja na malisho yake.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.