Mashangilio 57 - Swahili Roehl Bible 1937

Kuomba wokovu mikononi mwa wachukivu.Kwa mwimbishaji. Fumbo la Dawidi la kuimba kama wimbo wa kwamba: Usiangamize! Alilitunga alipomkimbia Sauli na kujificha pangoni.

1Nihurumie, Mungu! Nihurumie! Kwani roho yangu imekukimbilia wewe, kivuli kilichoko mabawani kwako nimekikimbilia, mpaka yaishe kupita mateso haya.

2Ninamwita Mungu alioko huko juu, ni yeye Mungu atakayenimalizia mashauri yangu.

3Atamtuma toka mbinguni atakayeniokoa, naye anifokeaye atamtia soni. Mungu hutuma upole wake nao welekevu wake.

4Hapa, roho yangu ilipotua, ni penye simba, nao wanipuliziao pumzi za moto ni wana wa watu, mikuki na mishale ni meno yao, nazo ndimi zao ndio panga zenye ukali.

5Utukuke, Mungu, juu mbinguni, nazo nchi zote ziuone utukufu wako!

6Miguu yangu waliitegea matanzi, nayo roho yangu wanaiinamiza. Walinichimbia mwina mimi, wakatumbukia humo.(8-12: Sh. 108:2-6.)

7E Mungu, moyo wangu umetulia na kushupaa, moyo wangu umetulia kweli na kushupaa; kwa hiyo na niimbe na kupiga shangwe!

8Amka, roho yangu yenye matukuzo! Amkeni, pango na zeze, niiamshe mionzi ya jua!Sh. 16:9.

9Kwenye makundi ya watu wako nitakushukuru, Bwana, nako kwenye wamizimu nitakuimbia.

10Kwani upole wako ni mkubwa, unafika mpaka mbinguni, nako mawinguni unafika welekevu wako.Sh. 36:6.

11Utukuke, Mungu, juu mbinguni, nazo nchi zote ziuone utukufu wako!

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help